Habari za Punde

Zanzibar Itaungana na Dunia Kuadhimisha Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani Disemba 3,2023

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu Salma Haji Sadat akionesha kitabu cha sheria za watu wenye ulemavu wakati akijibu maswali ya Waandishi wa habari akitoa taarifa kuhusiana na shughuli kuelekea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu ambayo hufanyika kila ifikapo Disemba 3 Duniani kote,hafla iliyofanyika Ukumbi wa Shijuwaza Mombasa Zanzibar.
Katibu Mtendaji Baraza la Taifa la watu wenye Ulemavu Zanzibar  Mhandisi Ussy Khamis Dede akijibu maswali ya Waandishi wa habari kuhusiana na shughuli kuelekea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu ambayo hufanyika kila ifikapo Disemba 3 Duniani kote,hafla iliyofanyika Ukumbi wa Shijuwaza Mombasa Zanzibar.
Mwandishi wa kituo cha Televisheni Zanzibar Cable Malik Shahraan akiuliza swali wakati wa utolewaji wa taarifa ya shughuli kuelekea maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu ambayo hufanyika kila ifikapo Disemba tatu Duniani kote, hafla iliyofanyika Ukumbi wa Shijuwaza Mombasa Zanzibar.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 

NA SABIHA KHAMIS, MAELEZO.

Makamu wa Kwanza wa Rais anatarajiwa kuwa mgeni rasmin katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Watu Wenye Ulemavu yatakayofanyika Disemba 03 ukumbi wa Polisi Ziwani.

Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Watu Wenye Ulemavu Salma Haji Sadati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na maadhimisho hayo amesema dunia huadhimisha siku hiyo kila mwaka kwa lengo la kuihamasisha jamii juu ya uelewa wa watu wenye ulemavu na kupata tathmini za upatikanaji wa fursa na haki ili kufikia malengo yanayojiwekea.

Amesema Zanzibar ni sehemu ya dunia hivyo wataungana na watu Ulimwenguni kuadhimisha siku hiyo ili kuhamasishwa jamii kujua  Watu wenye Ulemavu kutambua haki zao pamoja na kufikia malengo waliojiwekea.

                                                  

Amesema Baraza limejipanga kuzingatia mambo muhimu katika kuadhimisha siku hiyo ili kufikia maendeleo endelevu, hivyo ni vyema jamii ikaunga mkono jitithada zinazochukuliwa ili kufukia azma hiyo na kuondokana na vikwazo vinavyowakabili.

Alifahamisha kuwa Katika kueleke madhimisho hayo shughuli mbalimbali zilifanywa na Baraza la Taifa la watu wenye ulemavu  ikiwemo ziara ya kuhamasisha uwekaji wa mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu katika miundombinu ya barabara,majengo ya umma pamoja na kufanya bonanza la michezo kwa watu wenye ulemavu.

Madhimsho ya siku ya Watu wenye Ulemavu kwa mwaka huu yameambatana na kauli mbiu “Tuungane pamoja katika kuchukua hatua ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwa watu wenye ulemavu”

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.