Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Amewaapisha Viongozi Aliowateua Hivi Karibuni Viwanja vya Ikulu Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe,Ali Suleiman Ameir (Mrembo) kuwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu,kabla ya Uteuzi alikuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango,hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe,Mudrika Ramadhan Soraga kuwa  Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale,kabla uteuzi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Kazi,Kazi,Uchumi na Uwekezaji,hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe,Shaabani Ali Othman kuwa  Waziri wa Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi .kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Maji,Nishati na Madini,hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe,Juma Makungu Juma  kuwa  Naibu Waziri wa Nchi ,Ofisi ya Rais,Fedha na Mipango.kabla ya uteuzi alikuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi,Maendeleo ya Makaazi,hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe,Salha Mohamed Mwinjuma  kuwa  Naibu Waziri wa  Wizara ya Ardhi,Maendeleo ya Makaazi .kabla ya uteuzi alikuwa mwakilishi wa Viti maalum Kundi la Vijana Kusini,Unguja,hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi akimuapisha Mhe,Zawadi Amour Nassor kuwa  Naibu Waziri wa  Wizara ya Maji,Nishati na Madini .kabla ya uteuzi alikuwa mwakilishi wa Jimbo la Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar
Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na Mawaziri wapya walioapishwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia na kutoa maagizo kwa wateule hao  leo baada ya hafla kiapo iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.
Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM wakiwa katika   hafla ya kiapo kwa Viongozi walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kushika nyazifa mbali mbali, katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar.
Baadhi ya Viongozi wa Dini na Mawaziri na Maafisa katika Taasisi za Serikali wakiwa   katika hafla ya kiapo kwa Viongozi walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kushika nyazifa mbali mbali, katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar
Baadhi ya wanafamilia wa Viongozi walioapishwa wakiwa katika hafla ya kiapo kwa Viongozi walioteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kushika nyazifa mbali mbali, katika hafla iliyofanyika leo viwanja vya Ikulu Jijini Zanzibar
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.