Habari za Punde

Utiaji wa Saini Hati ya Mashirikiano ya Jeshi la Ulinzi Tanzania na Zambia

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dk. Stergomena Laurence Tax na Waziri wa mambo ya ndani na usalama wa ndani Zambia Norman Chipakupaku wakitia saini hati za ushirikiano katika maswala ya uhamiaji baina ya nchi hizo  katika mkutano wa pili wa kamisehni ya kudumu ya ushirikiano baina ya Wizara za ulinzi na usalama za Tanzania na Zambia. 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu)Mhe. Jenista J. Mhagama na Waziri wa mambo ya ndani na usalama wa ndani Zambia Norman Chipakupaku wakitia saini hati ya ushirikiano wa kupambana na matumizi ya madawa ya kulevya na usafishaji haramu wa binaadamu katika mkutano wa pili wa kamisehni ya kudumu ya ushirikiano baina ya Wizara za ulinzi na usalama za Tanzania na Zambia.

PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR 

Na Khadija Khamis –Maelezo .24/02/2024.

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergormena Lawrence Tax amesema hali ya ulinzi na usalama katika mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nchi ya Zambia iko salama


Aliyasema hayo katika Mkutano wa pili wa Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya Tanzania na Zambia katika sekta ya ulinzi na usalama huko Hotel ya Verde, Mtoni.


Amesema mkutano huo ni muendelezo wa mashirikiano juu ya hali ya kudhibiti ulinzi na usalama katika mipaka ya nchi hizo.

Ameeleza uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Zambia uko vizuri jambo ambalo linaongeza kuimarisha mashirikiano ya pamoja ikiwa ni muendelezo wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa Jamhuri wa Zambia.


Waziri Stergormena amefahamisha katika ziara hiyo hati za makubaliano takriban manane yamekubalika ikiwemo suala zima la ulinzi na usalama katika mipaka hivyo kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa.


Ameeleza kuwa licha ya kuwepo usalama katika mipaka lakini kuna matukio mengi ya ugaidi duniani ambayo yanayotokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.


Amefafanua kuwa kuna matukio mabaya ya usafirishaji wa biashara haramu ya binaadamu na dawa za kulevya na kupelekea kuwekwa mikakati ya pamoja ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo.


Waziri wa Ulinzi nchini Zambia Dkt Ambrose L.Lufuma amesema atahakikisha kuwa ushirikiano huo unaimarishwa hasa katika masuala ya ulinzi na usalama pamoja na ushirikiano wa kiuchumi.


Kikao hicho kimejadili ripoti za kamati ya ulinzi na usalama na kuweka msisitizo wa kuhakikisha azimio lililopitishwa linatekelezwa ndani ya muda uliokubalika.







No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.