Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Ameufungua Msikiti wa Masjid Al Abraar Tazari na Kujumuka Katika Sala ya Ijumaa Iliyofanyika Katika Masjid Hiyo

MUONEKANO wa Masjid Al Abraar Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja uliofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi, na kujumuika na Wananchi wa Kijiji cha Tazari katika Ibada ya Sala ya Ijumaa iliyofanyika leo 19-4-2024 katika Masjid hiyo
SHEHA wa Shehia ya Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja akizungumza na kutowa shukrani za Wananchi wa Kijiji cha Tazari, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari Mkoa wa Kaskazini Unguja leo 19-4-2024, wakati wa ufunguzi wa Msikiti huo uliofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi na kujumuika katika Ibada ya Sala ya Ijumaa.
MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wananchi kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi wa Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja leo 19-4-02024, katika hafla ya ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Tazari baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja uliyofanyika leo 19-4-2024
WANANCHI wa Kijiji cha Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza na kuwasalimia baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari, uliofanyika leo 19-4-2024.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi wa Kijiji cha Tazari katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi (kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe.Rashid Hadid Rashid, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na Ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari uliyofanyika leo 19-4-2024.
WANANCHI wa Kijiji cha Tazari Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja wakijumuika na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) katika kuitikia dua ikisomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Saleh Omar Kabi, baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na Ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari uliofanyika leo 19-4-2024.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Viongozi wa Masjid Abraar Tazari,baada ya kumalizika kwa Ibada ya Sala ya Ijumaa na Ufunguzi wa Masjid Al Abraar Tazari uliyofanyika leo 19-4-2024
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.