RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe.Dkt.Hassan Sheikh Mohamud, na kutowa mkono
wa pole kufuatiya kifo cha Baba yake Mzazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Awamu ya Pili Mstaafu Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, mazungumzo hayo
yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu
Ndogo Migombani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 28-4-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Rais wa Shirikisho
la Jamhuri ya Somalia Mhe. Dk. Hassan Sheikh Mohamud,
Ikulu ndogo ya Migombani, Zanzibar.
Katika mazungumzo yao, Rais Dk. Mohamud amempa pole
Rais Dk. Mwinyi kutokana na kifo cha baba yake mzazi, Marehemu Mzee Ali Hassan
Mwinyi, (Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania)
aliefariki dunia tarehe 29 Februari mwaka huu.
Rais Dk. Mohamud alikua ziarani nchini kwa siku mbili
kufuatia mwaliko rasmi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan hivi karibuni.
Pia, Rais Dk. Dk. Mohamud alihudhuria maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano wa Tanzania.
IDARA YA MAWASILIANO, IKULU ZANZIBAR


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiongozana na mgeni wake Rais wa
Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe.Dkt. Hassan Sheikh Mohamud, baada ya
kumaliza mazungumzo yao na kutowa mkono wa pole kufiatia kifi cha Baba yake mzazi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Mstaafu Hayati Ali Hassan
Mwinyi, mazungumzo hayo yaliyofanyika
katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Migombani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar
leo 28-4-2024
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Rais wa Shirikisho
la Jamhuri ya Somalia Mhe.Dkt. Hassan Sheikh Mohamud, baada ya kumaliza
mazungumzo yao na kutoewa mkono wa pole kufuatia kifo cha Baba yake mzazi Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Mstaafu Hayati Alhajj Ali Hassan
Mwinyi, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Ndogo Migombani
Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 28-4-2024
No comments:
Post a Comment