Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Mwinyi Amtembelea Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Bw. Hassan Rajab aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Zanzibar, alipofika nyumbani kwake Kisauni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja kwa ajili ya kumsalimia na kumjulia hali yake leo 10-5-2024.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Familia ya Bw. Hassan Rajab (kushoto kwa Rais) aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo yake alipofika nyumbani kwake Kisauni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja na (kushoto kwake) Ndg. Haji Kali, wakiitikia dua ikisomwa na Katibu Mtendaji wa Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh. Khalid Ali Mfaume (kulia kwa Rais)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Bw. Hassan Rajab aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Amani Zanzibar, baada ya kumaliza mazungumzo yake alipofika nyumbani kwake Kisauni Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 10-5-2024 kumjulia hali yake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.