
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
akitia saini kitabu cha maombolezo alipowasili nyumbani kwa Marehemu Mzee Hasanieli Mrema aliyeshiriki katika
tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar, mazishi yaliyofanyika
katika Kijiji cha Midawi, Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Serikali imesema itaendelea
kuuthamini na kuuenzi mchango wa wazee walioshiriki katika tukio la kihistoria
la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar.
Hayo yamesemwa na Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
wakati akitoa salamu za Serikali katika mazishi ya Mzee Hasanieli Mrema aliyeshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa
Tanganyika na Zanzibar, katika Kijiji cha Midawi Midawi, Wilaya ya Moshi mkoani
Kilimanjaro leo tarehe 08 Mei, 2024.
Amesema Marehemu Mzee
Mrema ambaye wakati alishiriki tukio hilo muhimu akiwa kijana wa umri wa miaka
20 akiwa na wenzake tarehe 26 Aprili, 1965 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es
Salaam mwaka mmoja baada ya Muungano enzi za uhai wake alikuwa tayari
kuzungumzia faida za Muungano huo.
Wengine watatu
walioshiriki tukio hilo la kuchanganya udongo ni Mzee Hassan Omari Mzee
kutoka Zanzibar, Marehemu Bi. Khadija Abasi Rashid kutoka Zanzibar na
Bi. Sifael Mushi kutoka Tanzania Bara.
Naibu Waziri Khamis
amesema marehemu alitoa wito kwa Watanzania hususan vijana kuulinda na
kuutetea Muungano na hata alipoombwa kuhojiwa na waandishi wa habari, hakusita
kufanya hivyo.
Mhe. Khamis ameungana na
waombolezaji kutoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu ambapo
amewasilisha salamu za pole kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Mhe. Khamis amesema marehemu
alishiriki katika Kongamano la Kitaifa la miaka 58 ya Muungano lililofanyika
Dodoma tarehe 26 Aprili, 2022 ambalo liliambatana na uzinduzi wa Kitabu cha
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Chimbuko, Misingi na Maendeleo, katika
tukio hili wenzake watatu hawakuweza kushiriki kutokana na changamoto za
kiafya.
“Tunamshukuru
sana Mwenyezi Mungu kwa maisha yake na tutazikumbuka nyakati zote ambazo
tuliweza kushiriki naye katika matukio muhimu ya kitaifa hususan sherehe za
Muungano ambapo yeye na wenzake watatu (Mzee Hassan, Bi. Sifael na Marehemu
Bi. Khadija) walishiriki kwa pamoja katika sherehe za Muungano
zilizofanyika Tanzania Bara (Dar es Salaam na Dodoma) na Zanzibar
pia,“ amesema Mhe. Khamis.
Naibu
Waziri Khamis ametoa rambirambi kwa familia ya marehemu kwa niaba ya Makamu wa
Rais Mhe. Dkt. Mpango na kusema kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu awape ngvu na
ustahimiloivu katika kipindi hiki kigumu.
Shughuli
hiyo ya mazishi hayo imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Zephania Sumaye
kwa aliyemwakilisjha Mkuu wa Kilimanjaro, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Muungano
Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Cesilia Nkwamu na viongozi wa wilaya..JPG)
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
akiungana na viongozi mbalimbali wa wilaya na waombolezaji katika katika
mazishi ya Marehemu Mzee Hasanieli
Mrema aliyeshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika na
Zanzibar, mazishi yaliyofanyika katika Midawi, Old Moshi mkoani Kilimanjaro
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
akitoa salamu za Serikali wakati wa mazishi ya Marehemu Mzee Hasanieli Mrema aliyeshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa
Tanganyika na Zanzibar, mazishi yaliyofanyika katika Midawi, Old Moshi mkoani
Kilimanjaro
Mkuu
wa Wilaya ya Moshi Zephania Sumaye akitoa salamu za Mkoa wakati wa mazishi ya
Marehemu Mzee Hasanieli Mrema
aliyeshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar,
mazishi yaliyofanyika katika Midawi, Old Moshi mkoani Kilimanjaro
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis
akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Mzee Hasanieli Mrema aliyeshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa
Tanganyika na Zanzibar, mazishi yaliyofanyika katika Midawi, Old Moshi mkoani
Kilimanjaro
Sehemu ya waombolezaji wakiwa katika mazisihi ya Marehemu Mzee
Hasanieli Mrema aliyeshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika
na Zanzibar, mazishi yaliyofanyika katika Midawi, Old Moshi mkoani Kilimanjaro
Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akiweka shada
la maua katika kaburi la Marehemu Mzee
Hasanieli Mrema aliyeshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika
na Zanzibar, mazishi yaliyofanyika katika Midawi, Old Moshi mkoani Kilimanjaro.

Sehemu ya waombolezaji wakiwa katika mazisihi ya Marehemu Mzee
Hasanieli Mrema aliyeshiriki katika tukio la kuchanganya udongo wa Tanganyika
na Zanzibar, mazishi yaliyofanyika katika Midawi, Old Moshi mkoani Kilimanjaro leo tarehe o8 Mei, 2024.
No comments:
Post a Comment