Habari za Punde

MRADI WA KIJALUBA WALETA NURU KUSINI UNGUJA.

Mratibu wa Mradi wa Kijaluba unaendeshwa na Tamwa Zanzibar kwa kushirikiana na SHIVIWAZA Hairat Haji akizungumza na Viongozi na Wanachama wa kikundi cha Watu wenye ulemavu cha Umoja ni nguvu (hawapo pichani) kuhusiana na mafanikio waliopata tokea kuanzishwa kwakwe huko Jambiani Mkoa wa Kusini Unguja.
Mratibu wa Mradi wa Kijaluba unaendeshwa na Tamwa - Zanzibar kwa kushirikiana na Shirikisho la Watu wenye ulemavu Zanzibar (SHIVIWAZA) Hairat Haji akizungumza na Viongozi na Wanachama wa kikundi cha Watu wenye ulemavu “Umoja ni nguvu” kuhusiana na mafanikio waliopata tokea kuanzishwa huko Jambiani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mratibu wa Mradi wa Kijaluba unaendeshwa na Tamwa - Zanzibar kwa kushirikiana na Shirikisho la Watu wenye ulemavu Zanzibar (SHIVIWAZA) Hairat Haji akizungumza na Viongozi na Wanachama wa kikundi cha Watu wenye ulemavu “Umoja ni nguvu” kuhusiana na mafanikio waliopata tokea kuanzishwa huko Jambiani Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

Na Takdir Ali. Maelezo. 13.06.2024.

Wanakikundi nchini wametakiwa kuitumia vizuri fursa wanazozipata ikiwemo misaada ili kuweza kufikia malengo ya kiuchumi waliojipangia.

 

Hayo yameelezwa na Mratibu wa mradi wa Kijaluba Khairat Haji wakati wa ziara ya kuangalia Vikundi vya Watu wenye ulemavu katika Mkoa wa Kusini Unguja.

 

Amesema lengo la ziara hiyo ni kuangalia mafanikio yaliopatikana katika vikundi hivyo, vinavyofadhiliwa Mradi wa Kijaluba, unaoendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA-ZANZIBAR) kwa kushirikiana na Shirikisho la Jumuiya za Watu wenye ulemavu Zanzibar (SHIVIWAZA) ili kuongeza ari na ufanisi katika utendaji.

 

Amesema wameamua kuunga mkono vikundi hivyo ili Watu wenye ulemavu waweze kujipatia kipato cha kuendesha Maisha yao na kuweza kujitegemea.

 

Aidha amesema hatua ya kuamua kuvisaidia vikundi hivyo ni kuunga mkono azma na mikakati ya Serikali katika kuwawezesha Wananchi kiuchumi pamoja na kuwapatia mitaji ya kuanzisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

 

Hivyo Khairat amewaomba Viongozi na Wanachama wa vikundi hivyo, kuyafanyia kazi maelekezo ya kitaalamu wanayopewa ili kufikia malengo yaliokusudiwa ya kuanzishwa kwa vikundi hivyo.

 

Kwa upande wake afisa Mwezeshaji wa vikundi vya kijaluba Muhiddin Ramadhani amesema wameweka utaratibu wa kukukutana na wanavikundi hao kila muda ili kubadilisha Mawazo na kubaini matatizo yaliopo na kuayatafutia ufumbuzi wa haraka. 

 

Hata hivyo wmewapongeza wanakikundi hao kwa ushirikiano wanaouonyesha jambo ambalo limepelekea kuimarika na kupiga hatua kimaendeleo na kufikia malengo ya kujikwamua na tatizo la umasikini.

 

Nao wanavikundi vya Watu wenye Ulemavu Mkoa wa Kusini Unguja wamesema wamefarajika sana kuanzishwa kwa vikundi hivyo kwani wameweza kupata mahitaji muhimu ikiwemo kulipia ada za Skuli kwa Watoto wao.

 

Hata hivyo wamesema wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mitaji midogo, vitendea kazi na ofisi za kufanyia kazi zao na kuwaomba waadhili na watu wenye uwezo kujitokeza kuwasaidia ili waweze kufikia malengo waliojipangia.

 

Ziara hiyo ya Waandishi wa habari na Tamwa – Zanzibar, kuangalia vikundi vya Watu wenye ulemavu Mkoa wa Kusini Unguja, imefanyika katika kikundi cha Mwanzo mgumu Michamvi, Nyota ya Bahati Bwejuu na Tutambuane Jambiani, ikiwa na lengo la kuangalia mapanikio yaliopatikana kwa kikundi hivyo tokea kuanzishwa kwake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.