Habari za Punde

MABALOZI, WENYEVITI NA MAKATIBU WA MATAWI JIMBO LA MFENESINI NA BUBUBU WAPEWA DOZI.

Na Takdir Ali. Maelezo. 01-07-2024.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi Kichama Fatma Ali Ameir amewataka Mabalozi, Mwenyeviti na Makatibu wa matawi wa Chama cha Mapinduzi kuyafanyia kazi kwa vitendo maagizo wanaoyopewa na Viongozi wao ili kuzidi kukiimarisha Chama na jumuiya zake.

Ameyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati alipokuwa akizungumza na Mabalozi, Wenyeviti na Makatibu wa UWT katika Jimbo la Mfenesini na Bububu kuhusiana na kuhamasisha Wanachama wa UWT kujisajili katika daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili na uandishaji wa wanachama wapya wa UWT.

Amesema viongozi hao ni nguzo imara katika Chama hivyo ni vyema kufanya kazi kwa bidii ili kuweza kufikia maendeleo endelevu na kuendelea kukiweka madarakani Chama cha Mapinduzi ifikapo mwaka 2025.

Aidha amewakumbusha kushiriki katika vikao na ili kujadili na kupanaga mipango ya maendeleo ya Chama hicho sambamba na kuendelea kutunza amani ya nchi iliopo kwani yanapotokea mafuriko wanaoathirika zaidi ni Wanawake na Watoto.

Kwa upande wake Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi kichama Mhe. Amina Iddi Mabrouk na Mwakilishi wa Viti maalum Kupitia Mkoa huo Mhe. Mwanaid Kassim Mussa amewataka Mabalozi kushirikiana na UWT katika kufanya usajili wa electronic ili kuweza kupata idadi kubwa ya Wanachama katika Mfumo.

Aidha wamesema kazi ya kukusanya takwimu ni ngumu hivyo amewataka kupendana na kushirikiana ili zoezi hilo liweze kufanikiwa.

Hata hivyo amewataka kuyatangaza mambo mazuri yanayofanywa na Viongozi wakuu wa kitaifa ili wananchi Wananchi waweze kuyafahamu na kuzidi kujenga Imani na Viongozi hao.

Mapema wakitoa michango yao Mabalozi,Wenyeviti na Makatibu wa UWT Jimbo la Mfenesini na Bububu wameomba kupewa kipao mbele katika mikopo na fursa za ajira wakati zinapotokezea.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.