Habari za Punde

WAZIRI WA UCHUMI WA BULUU NA UVUVI AZINDUA KAMPENI YA MKONO KWA MKONO AWAMU YA PILI ZANZIBAR.

Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Shaaban Ali Othman akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mkono kwa Mkono awamu ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni Zanzibar.

Na. Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.16/10/2024.

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalenga kuendeleza zoezi la ugawaji wa boti za uvuvi kwa kila Mkoa wa Unguja na Pemba ili kuisaidia jamii kujiwezesha kiuchumi.

Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Mhe. Shaaban Ali Othman wakati wa Uzinduzi wa Kampeni ya awamu ya pili ya Mkono kwa Mkono iliyofanyika Madinat Al  Bahari, Mbweni Zanzibar.

Amesema jumla ya boti 10 zitatolewa ambapo kila Mkoa Utapatiwa boti mbili ikiwemo ya  uvuvi na ukulima wa mwani kuisaidia jamii kujikwamua na hali ngumu ya maisha.

Amewataka wadau mbali mbali na wenye dhamana kutoa uelewa  kwa wananchi juu ya fursa za kiuchumi  zilizopo nchini ili wapate uelewa wa fursa hizo na kuzifanyia kazi.

Nae Mkurugenzi wa Wakala wa  Uwezeshaji wa Wananchi, Kiuchumi (ZEEA) Juma Burhani amesema Taasisi hiyo kwa kushirikiana na vyuo vikuu wanatarajia kuwawezesha vijana 15 hadi 20 kwa kuwapatia mafunzo ya ujasiriamali ili kuwainua vijana hao kiuchumi katika kujiajiri na kuajiri wengine.

Amesema kupitia kampeni hiyo wanategemea kuvipitia na kuvitambua viwanda mbali mbali vya Unguja na Pemba na kuwashajihisha wananchi kuvitumia viwanda hivyo.

“Mkono kwa Mkono wa msimu uliopita imewasaidia wananchi kupata mikopo baada ya kueleza changamoto zao” alisema Mkurugenzi  Burhan.

Kwa upanda wao Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) wamesema wataendelea kutoa taarifa na kuzisambaza kwa wananchi ili kuelewa miradi mbali mbali inayotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kampeni ya Mkono kwa  Mkono itaanzia Mkoa wa Kusini Unguja katika Ukumbi wa Dkt. Shein Tunguu siku ya Jumamosi Oktoba 19, 2024.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji Wananchi  Kiuchumi Juma Burhan Mohamed akizungumza kuhusu kuwawezesha wananchi katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mkono kwa Mkono Awamu ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji ZIPA Saleh Saad Mohamed akizungumza katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mkono kwa Mkono Awamu ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni Zanzibar.

Katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii Arif Abbas akizungumza kuhusu kuwapatia mafunzo Vijana kutatua changamoto zao  katika hafla ya Uzinduzi wa Kampeni ya Mkono kwa Mkono Awamu ya Pili hafla iliofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Madinatul Bahr Mbweni Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.