Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Mhe.Dk.Hussein Mwinyi amewasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe nchini Zimbabwe

Rais wa Zanzibar na Mwengekiti wa Baraza la Mapinduzi amewasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe nchini Zimbabwe na kupokelewa  Mwanasheria Mkuu wa Zimbabwe Mhe. Virginia Mabhiza pamoja na viongozi mbalimbali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mahmoud Thabit Kombo pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Balozi Simon Nyakoro Sirro.

Rais Dk.Mwinyi kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Viongozi Wakuu wa nchi Wanachama wa SADC utakaofanyika jijini Harare.

📅 19 Novemba 2024

📍Robert Gabriel Mugabe International Airport.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.