Mwanafunzi Lightness Enock akizungumza baada ya kumalizika shoo jinsi alivyofanikisha maandalizi hayo kwa kiwango kibwa kuonesha ubuni wake katika shoo hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mbabala Dodoma.
Mwanafunzi Lightness Enock Ngwangwalu mwenye umri wa miaka 16 aliyemaliza Kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Mbabala, Dodoma amesema ndoto yake ni kuwa mwanamitindo wa Kimataifa hivyo anaomba msaada kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Mwanamitindo wa Kimataifa Flaviana Matata ili aendelezwe hadi kufikia ndoto yake hiyo.
Alifikia kuomba msaada huo wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hii baada ya kuongoza vyema shoo ya wanafunzi wenzie waliovalia mitindo mbalimbali ya mavazi wakati wa mahafali ya 21 ya shule hiyo.
Mwanafunzi Lightness Enock (wa Tano kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi walioshiriki shoo ya mitindo ya mavazi iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mbabala Dodomo, wakati wa Mahafali ya 21 ya Shule hiyo.
Lightness Enock Ngwangwalu.
IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA MSIMAMIZI MKUU KAMANDA WA MATUKIO ONLINE TV
No comments:
Post a Comment