Na Abdi Suleiman, Pemba
TIMU ya Jamhuri, imefanikiwa kunyakua ubingwa wa Kombe la Maridhiano, baada ya kuibanjua Duma mabao 4-3 kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.
Baada ya dakika 90 za kukanyaga zulia la nyasi bandia katika uwanja wa Gombani, wanaume hao walikuwa wamefungana magoli 2-2, na kulazimika kuhukumiana kwa njia ya matuta.
Kabla kuingia hatua ya kupigiana penelti, mabao ya Duma yalifungwa na Ali Ramadhan (dk 37) na Madenge Khalfan (dk 68), huku yale ya Jamhuri yote yakifungwa na Ali Othman katika dakika za 64 na 66 mtawalia.
Wachezaji waliofunga penelti za Jamhuri walikuwa Mfaume Shaaban, Juma Othman, Mrisho Ahmed na Suleiman Ali Nuhu, huku Juma Ramadhan, Abass Rajab na Ali Ridhiwani wakiipacjhkia Duma na Sufi Saleh na Madenge Khalfan wakikosa penalti zao.
Kwa kutwaa ubingwa huo, timu ya Jamhuri ilizawadiwa donge la shilingi laki tano na kikombe, huku Duma ikikunja shilingi laki tatu na kikombe kidogo, ambapo kila timu iliyoshiriki michuano hiyo ilipewa mipira
miwili.
0 Comments