MKURUGENZI wa Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa Zanzibar (NIDA), Vuai Mussa Suleiman akifungua mafunzo
kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilivyopo Zanzibar kuhusiana na
zoezi la uandikishwaji wa vitambulisho vya taifa. Hapa anaonekana akitoa ufafanuzi
kuhusu ujazaji wa fomu ambayo itatumika wakati wa zoezi hilo.
Ofisa kutoka Idara ya Vitambulisho vya Taifa Tanzania Abdallah Mmanga, akitowa mada kuhusu Umuhimu wa Vitambulisho vya Taifa kwa Waandishi wa habari wakati mafunzo ya kuelimisha utoaji wa Vitambulisho na Umuhimu wake kwa Mtanzania na jinsi ya faida yake ili kumutambua Mtanzania na siyo Mtanzania anaeishi Tanzania.
Ofisa wa kutoka Idara ya Uhamiaji Zanzibar Chum .A.Kombo, akitowa elimu ya Uraia,UgeniUkaazi na Ukimbizi kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wa mafunzo ya Uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa, ambavyo kila Mwananchi anaiisha Tanzania ataandikishwa kutokana na vigezo hivyo na kutakuna na utafauti wa Vitambulisho, mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Chuo cha Amali Rahaleo.
Afisa wa Vizazi na Vifo Zanzibar Shaha Foum, akitowa maelezo jinsi ya upatikanaji wa Vyeti kwa Wananchi wa Zanzibar ili kufanikisha zoezi hilo la Uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa, ili kumuezesha kila mwananchi kuwa na Cheti cha kuzaliwa ili kuweza kuandikishwa katika zoezi hilo.
Waandishi wa Habari wa Vyomnbo mbalimbali vilioko Zanzibar wakiwa katika mkutano wa mafunzo ya zoezi la Uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa vya Tanzania jinsi zoezi hilo litakavyokuwa wakati wa uandikishaji kwa Wakaazi wa Zanzibar na Vitongoji vyake.
0 Comments