Hali ya hewa hivi sasa mjini Kiruna, Sweden haitabiriki, wakati mwengine theruji hudondoka kama inavyoonekana kwenye picha.
Afisa tawala wa wilaya ya Kusini, ndugu Abdalla Ali Kombo akimkabidhi picha ya kuchora meya wa Kiruna, bi Kristina Zakrisson. Picha hiyo yenye kueleza utamaduni wa watu wa Makunduchi mwaka kogwa imekabidhiwa baada ya mazungumzo ya mashirikiano baina ya Wadi za Makunduchi na Manispaliti ya Kiruna yaliyofanyika afisini mwa meya.
Mjumbe wa wadi za Makunduchi kutoka kamati ya elimu, mwalimu Hafsa Makame akipeana mkono na Meya wa mji wa Kiruna bi Kristina Zakrisson baada ya kumvisha mtandio wenye maneno: "HAKUNA MATATA ZANZIBAR" Aidha, ujumbe wa wadi za Makunduchi umetoa mualiko kwa meya wa Kiruna kutembelea Zanzibar.
Meya wa Manispaliti bi. Kristina Zakrisson amefurahia sana zawadi ya mtandio kutoka Zanzibar. Meya huyo ameahidi kuitembelea Makunduchi mwanzoni mwa mwaka ujao
Kutoka kushoto afisa tawala wa wilaya ya Kusini, Abdalla Ali Kombo, Moh'd Simba, Simai Ameir Haji, Meya bi Kristina, bwana Harold, Mohamed Muombwa, Mwatima Hassan, Hafsa Makame na Mwalimu Haji Kiongo. Sanamu inayoonekana katikati ni ya mwanzilishi wa mji wa Kiruna bwana Hjalmar Lundbohm ambaye amefanya mengi kwa watu wa Kiruna kiasi ambacho huwezi kuzungumza Historia ya Kiruna bila kumhusisha.
Wadi za Makunduchi zimekusudia kuanzisha kumbusho. Katika ziara yao mjini Kiruna ujumbe wa Makunduchi ulitembelea Kumbusho la wenyeji wa Kiruna waitwao "Sami" ambao maisha yao ni kama Wamasai; kuhamahama na mifugo kutoka sehemu moja hadi nyengine.
TMA Yabainisha Njia Rasmi za Kupata Taarifa za Hali ya Hewa
-
Na Mwandishi Wetu Michuzi Tv
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imebainisha njia rasmi zinazotumika
katika usambazaji wa taarifa za hali ya hewa nchin...
1 hour ago
0 Comments