Kontena likikaguliwa wakatika wa Makabidhiano ya Mtambo huo na Balozi Mdogo wa China Zanzibar Xie Yun Liang, katika viwanja vya Ofisi ya TRA Mlandege Zanzibar.
Waziri wa Fedha wa Zanzibar Omar Yussuf Mzee, akihutubia wakati wa sherehe za kukabidhiwa Gari Maalum laMtambo wa Kukagua Makontena Bandarini kutoka Serekali ya China, makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za TRA Mlandege Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China Zanzibar Xie Yun Liang, akizungumza wakati wa kukabidhi Gari Maalum la kukagulia makontena yanaoingia katika Bandari ya Zanzibar,
NAIBU Kamishna wa TRA Zanzibar Mcha Hassan, akizungumza katika sherehe hizo za uzinduzi wa gari maalum yenye mashine ya kukagulia makontena bandari ili kupata thamani halisi ya mzingo uliokuwemwe ndani ya kontena.MAOFISA wa TRA Zanzibar wakiangalia kabrasha la picha zinazoonesha utendaji wa kazi za Mtambo Maalum wa kuchunguza Makontena katika Bandari ya Zanzibar ili kudhibiti uhalali wa kulipia Ushuru wa Forodha kwa mizigio inayoingia Zanzibar kutoka nje ya Nchi.
Maofisa wa Ubalozi wa
WAZIRI wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee, na Balozi Mdogo wa China Zanzibar, Xie Yun Liang, wakitiliana saini makabidhiano ya Gari lenye mtambo wa kukagulia makontena yanayoingia Zanzibar kupitia bandari ya Malindi, mtambo huo una uwezo wa kumurika kili kitunkilimo katika kontena na kupata thamani hali ya mzingo uliokuwemo katika kontena hilo.
Balozi Mdogo wa China Zanzibar Xie Yun Liang, akizungumza na Waziri wa Fedha Zanzibar Omar Yussuf Mzee, wakati wa uzinduzi wa gari la Mitambo ya Kukagulia Kontena Bandarini, akitowa maelezi jinsi linavyofanya kazi gari hilo wakati wa makabidhiano yaliofanyika Ofisi za TRA Zanzibar.
WAFANYABIASHARA wa Zanzibar wakishuhudia uzinduzi wa Gari maalumu yenye mtambo wa kukagua makontena bandari wakiwa nje ya viwanja vya TRA Mabluu.
1 Comments
Kwa TRA hii iliyojaa mijizi. Wakiona hilo gari linawaletea noma kuendeleza kuiba wataliharibu kesho tu. Suala sio kua na teknolojia za kisasa Mh. Suala la msingi ni kudhibiti wizi mkubwa kwenye idara hii.
ReplyDelete