6/recent/ticker-posts

Amani Fresh yailaza Kilimani Stars 2-1

Na Mwajuma Juma
TIMU ya soka ya Amani Freshi imeanza vyema ligi daraja la pili baada ya kuifunga Kilimani Stars bao 1-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa Mao Tse Tung mjini hapa.

Mchezo huo ambao ulichezwa majira ya saa 10 za jioni ulikuwa na ushindani mkali kwa kila timu kutaka kuondoka na ushindi uwanjani hapo.

Ilichukuwa dakika 24 tu na timu ya Amani Freshi kupata bao hilo la pekee lililofungwa na Mtumwa  Mussa Makame bao ambalo liliwachanganya Kilimani Stars ambao walizidisha mashambulizi langoni kwa wapinzani wao lakini hadi mchezo huo unamalizika walijikuta wakiwa wamefungwa
bao 1-0.

Mbali na mchezo huo mapema kulifanyika mchezo kati ya Cozy Life na Dynamoo ambao ulimalizika kwa miamba hiyo kufungana bao 1-1.

Bao la timu ya Dynamoo ambao ndio waliotangulia kupata bao lilifungwa na Ibrahim Hassan dakikaya 42 na kusawazishiwa katika dakika ya 68 kupitia kwa mchezaji Rajab Jaffar.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa michezo miwili itakayochezwa kwenye uwanja wa Ziwani Polisi ambapo mchezo wa kwanza utachezwa wakati wa saa 8:00 kati ya Shangani na Vikokotoni na saa 10:00 Taifa ya Jang’ombe atavaana na Negro.

Post a Comment

0 Comments