6/recent/ticker-posts

Zantel yaandaa semina ya fursa kwa vijana Zanzibar

KATIKA kuhakikisha vijana wa Zanzibar nao wanapata nafasi ya kusikia fursa zilizopo na kuzitumia, Kampuni ya simu za mikononi ya Zantel imedhamini semina itakayofanyika Zanzibar kesho.
 
Semina hizo zitafanyika katika ukumbi wa Eacroternal, kuanzia saa mbili asubuhi kukiwa na wazungumzaji mbalimbali ambao watazungumza na vijana kuhusiana na fursa zinazopatikana Zanzibar na namna ya kuzitumia.
 
Baadhi ya wazungumzaji watakaotoa mada ni Ruge Mutahaba, (Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group), Mrisho Mpoto (msanii wa mashairi), Niki wa Pili (msanii wa Hip Hop) na wawakilishi kutoka tume ya sayansi na teknolojia pamoja na Mfuko wa Sekta Binafsi.
 
Semina za fursa ambazo mpaka sasa zimeenda mikoa 15 zinalenga kuhamasisha vijana kuchangamkia fursa zilizopo nchini, pamoja na kubadilisha mitazamo hasa ya kusubiri kufanyiwa mambo.
 
Semina hizo pia zinajadili mada mbalimbali kama ubunifu, ujasiriamali, uongezaji thamani kwenye bidhaa au shughuli yoyote unayofanya.
 
Akizungumzia kupelekea semina za fursa Zanzibar, Ofisa Biashara Mkuu wa Zantel, Sajid Khan, alisema kampuni yake imekuwa mstari wa mbele kuwawezesha vijana kupitia huduma na kampeni mbalimbali.
 
“Tanzania ina fursa nyingi sana kwa vijana na sisi Zantel tunaamini nafasi hii itakuwa muhimu kwa vijana kujifunza na kutambua fursa zilizopo na kuzitumia,” alisema Khan.
 
Chanzo - Tanzania Daima

Post a Comment

0 Comments