Na Abdalla Pandu
12/10/2013
Mjumbe wa Kamati kuu na Halmashauri kuu ya CCM ambae pia ni mlezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa mjini magharibi Shamsi VAuai Nahodha amewataka viongozi kujiamini katika kusimamia na kuelezea mafanikio ya nchi sambamba na kuwataka wana CCM kuchagua viongozi ambao watajali maslahi ya Taifa la Tanzania.
Amesema kuwa wakati huu ni wa kujadili changamoto zinazokabili ili kuzipatia ufumbuzi badala ya kutumia majukwaa kuanza kulaumu utendaji wa serikali.
Ilikuwa ni wakati wa mkutano wa kumtambulisha mlezi huyo wa mkoa wa mjini magharibi CCM katika kiwanja cha Baja maeneo ya Jangombe kisiwani Unguja.
Aidha amesema Tabia ya viongozi wa upinzani kuangalia matatizo ya Muungano peke yake ni udhaifu wakati Zanzibar ina changamoto nyingi za uvujaji wa mapato bila viongozi hao kuzungumzia wakati wengine ni viongozi kwa baadhi ya Sekta hizo.
Akizungumza wakati akimkaribisha mgeni Rasmin Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini magharibiBorafya Silima amesema kuwa Serikali ya mapinduzi itaendelea kuongozwa na waafrika waliopindua ukoloni katika mwaka 1964 hivyo Tamaa za baadhi ya viongozi kutamani kurejesha yaliopita katika ukoloni hilo haliwezekani.
Ikiwa Tanzania inaelekea katika kupata katiba mpya baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakiyatumia majukwaa ama vikao vyengine kushutumiana badala ya kuhubiri amani utulivu na hatua za maendeleo ya nchi.
1 Comments
nyinyi hamna mpya bwana, hamna la kuzungumza ila wapinzani hivi wapinzani hivi, kama kuna manufaa yoyote tuloyapata Zanzibar kutoka kwenye huo muungano au hiyo serikali yenu munafikiri wananchi hata wangewasikiliza hao wapinzani wanawasikiliza kwasababu nyinyi hamna hata kimoja cha maana tunachokiona sasa tufanye nini tutawaunga mkono haohao, hamna ila amani na utulivu nchi ngapi hazina muungano na kuna amani kuliko hapo znz juzi tu hapa tumemuona askari anavyompa mtu kipigo, nyinyi serikali mshapiga watu mara ngapi, kuna watu wangapi jela hawana hata kesi leo yangapi? tunaona vikosi vyenu SMZ vikidhulumu watu hivi hivi, ndo amani na utulivu wenu huo?
ReplyDelete