Na Munir Zakaria
Sheikh Azan Khalid Hamdan leo anatarajia kukutana na Daktari baada ya kumaliza hatua ya kwanza ya kufanyiwa vipimo vyote muhimu ikiwemo Full Blood Picture.
Sheikh Azan ambaye amefuatana na Mama watoto wake pamoja na Daktari kutoka hospitali ya Mnazi Mmoja (Dk.Rashid Ahmed) amesema amefika salama nchini India na anatarajia kukutana na Daktari baada ya kukamilisha vipimo vyote.
Sheikh Azan amesema kwa yeyote mwenye kutaka kumjulia hali na kumuombea dua anaweza kuwasiliana naye moja kwa moja kwa kutuma ujumbe mfupi kupitia namba +91 9916834792.
"Naomba wale wote wenye kutaka kuwasiliana na mimi wanitumie ujumbe mfupi(sms) kupitia namba yangu +91 9916834792 naomba wasinipigie simu bali watume ujumbe mfupi kupitia namba hiyo" alisema Sheikh Azan katika taarifa yake fupi aliyoituma baada ya kuwasili salama nchini India.
Amesema lengo la kuwataka waislamu kumtumia ujumbe mfupi badala ya kumpigia simu ni kumwezesha kupata matibabu kwa utulivu katika kipindi hiki kigumu kwa vile wakati wowote anaweza kufanyiwa upasuaji.
"Inshallah nitakujulisha kila hatua ninayoendelea katika matibabu yangu, naomba ufikishe ujumbe huu kwa ndugu zangu wote wa Kiislamu" alisema Sheikh Azan.

0 Comments