Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muuungano wa
Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete, amemteua, Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa
Mashitaka (DPP) nchini.
Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar
es Salaam jana na Kaimu Katibu Mkuu
Kiongozi, Bwana Peter Ilomo, imesema uteuzi huo umeanza Ijumaa ya Oktoba 3,
mwaka huu.
Kabla ya uteuzi huo, Mganga
alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa
Serikali Mfawidhi.
Mganga anachukua nafasi ya
Dk.Eliezer Feleshi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara hiyo.
0 Comments