Kabla ya kuchukua uamuzi huu mzito
Ambao kwa kiasi kikubwa kuathiri maisha yako ambayo mlitarajia kuwa na maisha mazuri yaliyojaa raha, huba na mapenzi yasiyo kifani.
Ambao unaweza kutengua ahadi, malengo na matumaini ambayo mlikubaliana wakati mkifunga ndoa.
Ambao utawaondosha katika ile hali ya kuwa na staha na heshima ya hali ya juu kwa kuwemo katika chuo adhimu cha ndoa na kubaki wajane au wataliki.
Umewahi kukaa na kutafakari maisha nje ya ndoa yako vipi? Je utampata mwengine ambaye atakuwa na sifa na vigezo ambavyo umeona vimekosekana au kutokuwepo kwa uliye nae?
Unadhani utaweza kufunguliwa mlango mwengine ukienda kugonga kupeleka au kuletwa posa hasa ikiwa tayari umeshajitia doa.
Umewahi kutafakari kwa kina na kituo ni kipi hasa kilichokupeleka kutaka kuchukua uamuzi huu au ni hasira tu na maudhi yasiyokwisha?
Unakumbuka mlipoamua kuoana mliridhiana, mkakubaliana na mkawafikiana Je mlikuwa na haraka? Au mlipanga mkapangua, mkawaza mkawazua mpaka mkafikia sauti moja na kauli moja? Kwanini sasa hamtaki kupitia mfumo ule ule mliotumia kabla ya kuoana?
Umewahi kurudi kwa Allah Subhaanahu Wata’ala na kutaka mwongozo nini ufanye wakati Allah Subhaanahu Wata’ala ndiye mwenye kuzilinda ndoa zetu?
Labda nikukumbushe tu baadhi ya mambo ambayo ima hudaiwa au hutolewa talaka kisha nitakuuliza
Ugomvi na Kutopatana
Hali ngumu ya uchumi (maisha magumu)
Matatizo ya kifamilia
Kutoka nje ya ndoa kwenda kufanya uzinzi
Matatizoya kibailojia (ugumba, utasa)
Mapenzi kutoweka na kubaki mazoea
Kuingiliwa na ndugu na jamaa
Kutoaminiana
Ndoa za kulazimishwa (mkeka, kukamatiwa)
Je katika baadhi tu ya haya mambo yaliyotajwa ni kweli suluhisho lake la mwisho ni talaka?.
Tuchangie
Hapo keo umetugusa katika yale matatizo yanayosumbua maisha na famillia zilizo nyingi katika maisha yetu ya leo, tunaomba mada kama hizi nazo zipate nafasi tusijitupe sana kwenye siasa tukasahau mambo ya jamii yakila siku, asante mwandishi na hongera kwa kutafakari na kujua nini jamii inahitaji.
ReplyDeleteIla niongezee kidogo miongoni mwa mambo yanayo sababisha ongezeko la kuvunjika kwa ndoa ni ukosefu wa elimu ya ndoa, kwakawaida wengi wetu tunjiingiza tu bila ya kupata taaluma yoyote inayohusu maisha hayo, kwahivyo tunakosa uwezo wa kuziendesha ndoa zetu na ndiomana zinavunjika kiholela.
send for michuzi blog watu wengi watachangia
ReplyDeleteASalaam Alaiku, Mie nikijana mdogo ili suhala ni la kweli kabisa Nafikiri Tuanze kujuwa Dini na Kwenye Dini kupeleka Wake zenu Darsa la Dini na Sie kwenda kwenye dini tukishaanza kuogopa ya Allah, na kujuwa Watu wa Dini walifanya nini na wake zao basi njia ni nyepesi. MZ.
ReplyDeleteMchangiaji wa kwanza amegusia nukta muhimu ya ukosefu wa elimu ya ndoa.
ReplyDeleteJe kuna mkakati au program yoyote mtu anaweza kufikiria ili tuweze kufikisha elimu? Au ni wanandoa wenyewe ndio not interested na elimu hiyo?