Habari za Punde

KOMBAINI YA BENKI YAIBUKA KIDEDEA KATIKA BONANZA LILILOANDALIWA NA BENK YA POSTA TANZANIA KWA KUIFUNGA TIMU YA WAJUMBE WA BARAZA LA WAWAKILISHI ZANZIBAR VIWANJA VYA MAO DZEDONG.

MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba. K .Moshingi, alipowasili katika viwanja vya Mao Dzedung katika Tamasha la Bonaza la Mabenki Zanzibar lililoandaliwa na Benki ya Posta Tanzania.katikati Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Bihindi Hamad.    
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya Sira Mwamboya., akitabasamu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Sabasaba K.Moshingi.   
MABINGWA wa Bonaza la Mabenki ya Zanzibar wakishangilia ubingwa wao baada ya kuifunga timu ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, katika bonaza lililoandaliwa na Benki ya Posta Tanzania kwa Wafanyakazi wa Benki zilioko Zanzibar.
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd akimkabidhi Kikombe cha Ubingwa wa kufuta kamba Nahodha wa timu ya Wawakilishi Hamza Hassan baada ya kuwashinda watunza mapesa wa mabenki.
Mjumbe wa Barazaa la Wawakilishi Mgeni Hassan Juma akimkabidhi kikombe cha ubingwa wa Bonaza la Mabenki Nahodha wa timu ya Kombaini ya Benki Abdull Mshangama wa benki ya KCB.baada ya kuifunga timu ya Wawakilishi kwa peneti 5 - 6.mchezo uliofanyika uwanja wa Mao Dzedung. 
MAKAMU wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba K Moshingi wakitoka kukagua timu wakati wa mapumziko ya kipindi cha kwanza.   
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba K Moshingi wakiwasalimia wachezaji wa  timu ya Wawakilishi wakatik wa mapumziko wa mpambano huo ulioamuliwa kwa mikuju ya peneti.    
Mchezaji timu ya Kombaini ya Benki Abdull Mshangama akimtoka mpizani wake mchezo wa bonaza.   
MSHAMBULIAJI wa timu ya Kombaini ya Benki Mohammed Himid akimpita beki wa timu ya Wawakilishi wa Micheweni Subeit Khamis Faki, katika mchezo wa bonaza lililoandaliwa na Benki ya Posta Tanzania.    
Mheshimiwa wa Micheweni Subeit Khamis Faki na Mchezaji wa Kombaini ya Benki Mohammed Himid wakiwania mpira.  
MCHEZAJI wa timu ya Kombaini ya Benki Juhudi Othman kulia akimpita kiungo mchezeshaji wa timu ya Waheshimiwa Abdalla Mohammed Ali  (Jimbo la Mkoni) katika mchezo wa bonaza uliofanyika uwanja wa Mao Dzedung.    
MHESHIMIWA wa jimbo la Mtoni Nassor Mazrui akimpita mxchezaji wa timu ya Kombaini ya Benki Haji Dau. 
HIVI ndivyo ilivyokuwa wakati wa mchezo wa kukata na shoka wa bonaza la Kombaini ya Benki na Waheshimiwa Mheshimiwa wa  Micheweni Subeit Khamis akijaribu kumzuiya mshambuliaji wa timu ya Kombaini ya Benki  mwenye mpira Mohammed Hassan, mchezo huo umeamuliwa kwa matuta hatimai timu ya Kombaini ya Benki imeshinda 6-5.
WACHA ndivyo inavyoonekana beki huyu wa timu ya kombaini ya Benki.
WAANDISHI wa habari wakifuatilia Bonaza la Timu ya Kombaini ya Mabenki ya Zanzibar lililoandaliwa na Benki ya Posta Tanzania.
MLINDA mlango wa timu ya Wawakilishi Jaku Hashim akiruka bila ya mafanikio kujaribu kuokoa peneti
WAPENZI wa mchezo wa mpira wakiwa katika mpambano wa Bonaza uwanja wa Mao Dzegun.
WAFANYAKAZI wa Mabenki wakishangilia timu yao ikitolewa jasho na Waheshimiwa Wawakilishi katika mchezo wa Bonaza la Mabenki lililoandaliwa na Benki ya Posta Tanzania.
WAHESHIMIWA wakifuatilia mchezo wao na timu ya Kombaini ya Benki za  Zanzibar, uliofanyika uwanja wa Mao.
WATUNZA Fedha wa Mabenki Zanzibar wakijipima nguvu na Waheshimiwa Wawakilishi katika mchezo wa kuvuta kamba timu ya Waheshimiwa imeibuka mshindi wa mchezo huo. 
WAHESHIMIWA wakitunisha misuli wakiwavuta Watunza Pesa wa Benki katika mchezo wa Bonaza la Mabenki.na kutoka washindi wa mchezo huo.
KIONGOZI timu ya Wawaklilishi Dau Hamadi akitete na Mratibu wa Bonaza hilo Meneja wa Benki ya Posta Zanzibar.
WAKIKIMBIZA Kuku kwa upande wa Wanawake mshindi wa mbio hizo ni Waheshimiwa Wawakilishi.   
WAFANYAKAZI wa Mabenki wakiwa na kuku wao baada ya kumkamata katika mchezo wa kukimbiza kuku.kwa Wanaume
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba K Moshingi akimpongeza kipa wa timu ya Waheshimia Jaku Hashim kwa jitihada zake za kulinda goli lake. 
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Posta Tanzania akizungumza na Waandishi wa Habari  baada ya kumalizika kwa michezo ya Bonaza ilioandaliwa na Benki yake jinsi ilivyofana kuwa karibu na wateja wao katika sekta mbalimbali za maendeleo.    
MKURUGENZI mTENDAJI wa Benki ya Posta Tanzania Sabasaba K Moshingi akifurahia jambo na Waandishi wa Habari baada ya kumalizika kwa Bonaza hilo uwanja wa Mao. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.