Habari za Punde

WIGO UNACHANGIA MMOMONYOKO WA MAADILI

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Abdillahi Jihad Hassan, amesema jambo linalochangia mmong’onyoko wa maadili kwa watoto ni tabia ya watoto kupenda kuiga.

Aidha alisema kupungua kwa kasi ya wazazi kuwaonya watoto wao pale wanapoanza kubadili tabia kufanya mambo hayo ni tofauti na utamaduni wa Kizanzibari ili kuyadhibiti hayo ni vyema kurudia malezi yetu ya asili ambapo mtoto hulelewa na jamii.

Waziri Jihad alisema hayo alipokuwa akijibu suali la Jaku Hashim Ayoub (Muyuni), aliyemuuliza Waziri kuwa Sekta ya utalii inachangia kwa kiais kikubwa katika kummongonyoko kwa maadili hasa kwa watoto wadogo, jee Serikali ina mtizamo gani juu ya suala hilo.

Waziri Jihad alisema hadi sasa hakuna utafiti uliofanywa ambao unaonesha kuwa utalii unachangia kwa kiasi kikubwa lakini kumong’onyoka kwa maadili ka vijana hilo halihusiani moja kwa moja na utalii.

Alisema kuna mambo mengi yanayochangia kumong’onyoka kwa maadili ikiwemo suala la utandawazi na kukua na kukua kwa matumizi ya sayansi na teknolojia.

Sambamba na hayo alisema kwa kuzingatia umuhimu wa utamaduni na maslahi kwa watoto Serikali imeunda kamisheni ya utamaduni iliyopewa jukumu la kusimamia utamaduni wa Mzanzibari na kuhakikisha kuwa unalindwa na kuhifadhiwa na idara inayoshughulikia masuala ya vijana na watoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.