Habari za Punde

AJALI LATEST UPDATES

Serikali imewazika watu 17 katika makaburi maalum eneo la Kama hivi usiku baada ya miili yao kuharibika vibaya na kutoweza kutambulika kirahisi na hivyo hazikuweza kulazwa.

Waliofariki mpaka hivi sasa tunavyorusha taarifa hizi ni 192 wengi wao ni watoto wadogo na majeruhi 612 ambao wengine bado wamelazwa Hospitali za Kivunge na Mnazimmoja na wengine wameweza kuruhusiwa kurudi majumbani .

Harakati za uokoaji zitaendelea kesho na mpaka sasa haijulikani ni watu wangapi waliobakia.

Serikali imetangaza siku tatu za maombolezo na shughuli zote nyengine zimesitishwa.

2 comments:

  1. Asalamu alaykum
    Kwa kweli msiba mkubwa ila ni mipango yake Allah

    Pia naipongeza serikali yetu kwa juhudi zake za dhati kabisa, kwani juu ya uwezo wetu mdogo wa resource lakini Serikali pamoja na wananchi tumeonesha moyo wa kujitolea kwa kushajihishwa na serikali yetu, matokeo ya manusura wengi kiasi hichi ni mfano tosha wa mafanikio ya serikali juu ya Jambo hili.
    Allah awazidishie viongozi wetu moyo wa kutujali

    Ameen

    Abubakar

    ReplyDelete
  2. Jamani, mimi nna mashaka kidogo na idadi halisi ya waliofariki dunia hadi sasa, Kwenye TVZ. tunaziona maiti zikiwa na namba hadi 378,lkn. serikali inatuambia hadi sasa ni 192 vipi hapa? au wamezitia namba kama vile vyumba vya mahoteli? maana hoteli utaiona na vyumba 20 tu,lkn. funguo zake, zimeanza na 101-120...msaada tutani..wazee!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.