Habari za Punde

WASHAURI TAIFA STARS IWAACHIE ZANZIBAR HEROES

Pamela Chilongola

BAADHI ya askari polisi walioko Kibaha, Pwani wamelitaka Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, iipe nafasi timu ya taifa ya Zanzibar kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya kimataifa kwa kuwa inaonekana kuna mipango.

Wakizungumza na Mwananchi kwa sharti la kutotajwa majina kutokana na kazi yao, walisema wamechoshwa na kushindwa mara kwa mara kwa Tanzania katika michuano mbalimbali.


"Hivi katika miaka 50 ya Uhuru, tutajivunia kipi hasa, angalia wenzetu Ghana, kila mwaka wanafanikiwa, Nigeria, Afrika Kusini leo tutasema nini," alisema askari mmoja.

Mwingine alidakia kusema: "Kwanini wasiwaachie wa Zanzibar ili na wao wapate bahati yao, tunashangaa kuona TFF inapoteza fedha nyingi kugharamia timu yetu ya taifa na matokeo yake wanaishia kukwea pipa tu.

“Umefika wakati sasa kutoa nafasi kwa Zanzibar kuwaacha kuandaa timu ya taifa nasi kuwa watazamaji ili tuone nao matunda yao kwani ukitazama wachezaji wanao cheza timu za Ligi Kuu ya Bara ni wengi lakini katika timu ya Taifa ni wachache sasa hapa kunanini? Huoni kama tunawabana?

"Kama JKT Oljoro ya Arusha, Azam FC, Mtibwa Sugar, Coastal Union ya Tanga na timu zingine wote wanacheza vizuri tena katika vikosi vya kwanza lakini hawajulikana kama ni wachezaji sasa kama tunawabana tuwaache waendeze timu yao na wao.

“Kuna wachezaji wengi wa Zanzibar wako nje ya nchi wanachezea klabu mbalimbali lakini hawajulikani...kule Zanzibar mpira wanaucheza kama ni starehe halafu kiwango chao kipo juu laiti TFF wangewanyanyua nadhani kiwango chao kingekuwa kipo juu sana,” walisema .

Chanzo: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.