Na Asya Hassan
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai amewataka viongozi wa Jumuiya ya Wazazi kushirikiana pamoja katika kutekeleza ilani ya chama hicho ili waweze kukipatia ushindi ifikapo 2015.
Alieleza hayo alipokuwa akifungua kongamano la wazazi Mkoa wa Mjini Magharibi lililofanyika katika ukumbi wa ofisi kuu ya CCM Kisiwandui.
Alisema umoja na mashirikiano ndio njia pekee ambayo itawezesha kukipatia ushindi wa kishindo chama hicho.
Alisema kuwa jumuiya ya wazazi ndio muhimili mkubwa katika usimamizi wa kukipatia ushindi chama hicho na kuwaomba wanachama waache tofauti na kasoro zao ambazo zitasababisha kukipunguzia kura chama hicho.
Naibu huyo alisema kasoro mbalimbali zilizojitokeza katika uchaguzi uliopita ndio zilizosababisha kukipunguzia kura chama hicho.
Alifahamisha kuwa hivi sasa ni wakati mzuri wa kutafuta njia mbadali ili kukabiliana na uchaguzi ujao wa mwaka 2015 na kutaka kuwa makongamano hayo yasiishie katika mkoa wa mjini magharibi yaendelee na
sehemu nyengine kwani itawasaidia katika kijipanga zaidi.
Hata hivyo, alitumia fursa hiyo kwa kuwataka viongozi wa majimbo kushirikiana katika kutekeleza ilani ya chama majimboni mwao na sio kuwasikiliza watu ambao huwa wanaongoza kwa kueneza kasumba zisizo na
maana.
Alifahamisha kuwa wapo baadhi ya watu ambao hujifanya wao wapambe wa viongozi hao na kazi zao kuwatia kasumba ambazo zinasababisha kurejesha nyuma maendeleo ya jimbo na chama
HAYA MASUALA TUMEYAWEZA,ISIPOKUWA TUMEBAKIA KIDOGO TU ULE UBINAFSI WETU WA ROHO WA MAZOEA YETU YA ZAMANI,LAKINI SISI WAZANZIBAR SIKU ZOTE TUNA TABIA YA UUNGWA SANA,HATA SISI TULIOKU ULAYA WATU WOTE WA TAIFA LOLOTE ANAPOKUTANA NA SISI HUA ANAONA KUWA TUNA TABIA ZA PEKEYETU ZA KIUNGWANA AMBAPO NI ADIMU KWA SASA DUNIANI KUPATIKANA,NI MIAKA MINGI SASA WAZANZIBAR WOTE WALIOKO NJE YA NCHI KILA WANAPOULIZWA WATAPOTOKEA WANAKUWA WANAKATAA KATU KUWA WANATOKA TANZANIA BALI WANASEMA MOJA KWA MOJA KUWA WANATOKEA ZANZIBAR,KWANI KUNA TABIA ZISIZO FANANA KATI YA BARA NA WAZANZIBAR,KUTOKANA NA WAZANZIBAR HAO PAMOJA NA KUWA NI MIAKA MINGI HATA KABLA YA KUONDOKA KWA NYERERE WALIKUWA NA MSIMAMO WAO HUO HUKU WAKIJUA IPO SIKU WAKISEMA TU HUKO NJE WALIKO WATU WATAWEZA KULIJUA KUWA TAIFA LA WAZANZIBAR LINA WATU WAUNGWANA NA WENYE DESTURI NZURI,KWA MAONO YETU HUKU NJE NI KUWA HIVI HAPO NYUMBANI SISI KAMA SOTE NI BINAADAMU NA KILA BINADAMU ANAKUWA ANAKOSEA,KWAHIO NIKUWA TUMEKOSEANI KIDOGO TU KISIASA ZILE ZILIZOTUTANGULIA KABLA,SIASA AMBAZO ZILITUDHOOFISHA NA KUONDOA FURAHA,UDUGU NA UTU WETU KWA FITNA ZA SIASA ZA NDUGU ZETU WA BARA AMBAO WALIKUWA WAKITULETEA VIFARU NA MAJESHI YAO ILI YAJE KUTUUA NA PIA KUTAKA SISI WENEYEWE KWA WENYEWE TUUANE NA KUHASIMIANA KUTOKANA NA NA FITNA ZILIZOPANDIKIZWA KATIKA JINA LA SIASA ZA TANZANIA.
ReplyDeleteIMEFIKIA WAKATI WAKATI KWA UPANDE WETU WANZANZIBAR TUIJENGE NCHI YETU AMBAYO TUNAO UWEZO MKUBWA WA KUIJENGA SANA KULIKONI NDUGU ZETU WA BARA KWANI WANA KAZI KUBWA YA KUIFANYA KUIFANYA KWAVILE MAUVU YOTE KUANZIA ,UJAMBAZI,RUSHWA,WIZI WA SERIKALINI WAO NI WENGI SANA NA NCHI YAO HAIPO KTK CONTROL YOYOTE YA KUWEZA KUYAONDOA MACHAFU YOTE KULE BARA TOFAUTI NA SISI VISIWA VYETU TUKIAMUA TU BASI HAKUNA UCHAFU WOWOTE AMBAO UTAINGIA NDANI NA ULIKUWEPO NDANI NI RAHISI KWETU KUUSAFISHA,KWANI MABALA YA UNGA KWA VIJANA WETU PAMOJA NA MENGINE MINGI TUTAWEZA KUYAFANYIA KAZI KUBWA YASIWE NA NAFASI YOYOTE KTK MIPAKA YETU.
HIVI NDUGU ZANGU IMEFIKIA MUDA WA KUSAMEHEANA NA KUONDOA TOFAUTI ZETU ZA KIKABILA,RANGI,VYAMA VYA SIASA ILI TUWEZE KUIJENGA NCHI YETU.
HIVI SASA IMEFIKIA MUDA KAMA TUKITAKA HASA BASI BINADAMU WOTE WOTE HAPO NYUMBANI WATAKUWA TAYARI HATA KAMA SERIKALI ITATANGAZA SIKU ZA WANANCHI WAKE WAJITOLEE KUJENGA TAIFA KAMA MIAKA YA ZAMANI BASI WANANCHI WATAKUWA TAYARI KUFANYA HIVYO,HAKUNA KITU KIZURI ZAIDI CHA MAENDELEO ZAID KULIKO UMOJA,NA HAKUNA KITU KIBAYA ZAIDI DUNIANI KAMA MFARAKANO NA UTENGANO ,HATA KATIKA FAMILIA KAMA KUTAJITOKEZA BAADHI YA WATU WANAJITENGA BASI HAPO NDIO UTAKAPOANZA MPASUKO NA MFARAKANO NA MAISHA KUANZIA HAPO YATABADILIKA KUWA KATIKA HALI MBAYA HATA KAMA MTU ATAKUWA NI MILIONEA,KWANI HATA HUKO MAREKANI NA ULAYA MATAJIRI WAKUBWA MAISHA YANAWASHINDA KUTOKANA NA KUWA NA MATATIZO MENGI YA KFAMILIA AU YA KIMAPENZI KUTOKANA NA HUO MFARAKANO AIDHA HUTOKANA NA FITNA KATI YAO ZILIZOANZISHWA AU ALIZOZIANZISHA MOJA WAO.
IMEFIKIA MUDA HIVI SASA NDUGU ZANGU WA ZANZIBAR TUSAMEHEANE NA KUREJESHA UMOJA WETU NA KUWA NA FURAHA KATIKA NYUSO ZETU,TUNACHOKIHITAJIA HIVI SASA NI KITU KIMOJA TU AMBACHO KINAWEZEKANA KABISA ILI KUWEZA MOJA KWA MOJA KUWA NI WAZANZIBAR,ILIKUWEZA KUIFIKIA HATUA HII INAYOWEZEKANA KABISA NI KUVIUNGANISHA VYAMA VYETU VYOTE VYA ZANZIBAR NA KUIFANYA ZANZIBAR KUWA NI MOJA NA NGUVU ZA DOLA NA HAPO FURAHA YETU ITAREJEA KAMA ZAMANI NA MAMBO YA VYAMA ITAKUWA NI KUWAPATA WAWAKILISHI TU NA SIO KUWANIANA MADARAKA YA URAIS AMBAPO KATI YA VYAMA VIKUBWA VITAKAVYOKUWA VIKISHINDA KTK KURA ZA BUNGE LETU LA UWAKILISHI VITAKUWA VIKICHUKUA NA KUPOKEZANA HIZO NAFASI ZA URAIS "YAANI MUUNGANO WA WAZANZIBAR"AMBAPO TUTAWEZA KUUA ZILE FITNA KUTOKA KWA NDUGU ZETU-YAANI MAJIRANI ZETU WA BARA, (KWA KIFUPI BARA NI MAJIRANI ZETU)NA MARA NYINGINE UNAMLETA JIRANI NYUMBANI KWAKO NA UKAMUONYESHA MKE WAKO/MUME WAKO BAADAE AKAANZA KUKULETEA FITNA NDANI YA NYUMBA YAKO NA KUANZA KUFARAKANA NA MKE/MUME WAKO NA WATOTO WENU,NDIO HAWA MAJIRANI ZETU WA BARA WALIVYO NA WANAVYOFANYA KWETU.