Habari za Punde

ZANZIBAR HEROES YABWAGWA 2-1 NA WANYARWANDA




 

Abdulham Gulam akipambana na Kagere Medie wa Rwanda kwenye mchezo wa Robo Fainali ya pili kwa siku ya leo ikiwa ni michuano ya kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 inayofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Tanzania. mpaka sasa mpira umekwisha ambapo Rwanda imeongeza goli la pili katika dakika ya 86 na kufanya matokeo ya mchezo huo kwa magoli 2-1. Matokeo haya yanaifanya Zanzibar Heroes kufungasha virago na Watanzania kubakiwa na timu moja tu ya Kilimanjaro Stars ambayo itashuka dimbani kesha kuikabili Malawi.

Wazir Salum wa Zanzibar Heroers akijaribu kumzuia Ntamuhanga Tumaini wa timu ya Rwanda Amavubi katikamchezo wa robo fainali uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii

Picha na Fullshangwe. Blog

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.