Habari za Punde

Ibrahim Mzee Mkurugenzi Mpya wa Mashtaka (DPP)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein leo amefanya uteuzi wa Viongozi katika Taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kwa mujibu wa Taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk Abdulhamid Yahya Mzee imeeleza kuwa kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 56(1)(a) cha katiba ya Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein amemteuwa Ibrahim Mzee Ibrahim kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar. 


Kabla ya Uteuzi huo Ibrahim alikuwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na ana Shahada ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. 

Aidha Dk Shein kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 5(1) cha sheria ya Ofisi ya Mufti Namba 9 ya 2001 amemteuwa Sheikh Mahmoud Mussa Wadi kuwa Naibu Mufti. 

Pia kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu 3(1) cha sheria ya Vizazi na Vifo Namba 10 ya 2006 Dk Shein amemteuwa Shaaban Ramadhan Abdulla kuwa Mrajis wa Vizazi na Vifo. 

Ramadhan ana shahada ya sheria. Aidha kwa uwezo aliopewa chini ya kifungu 4(1) cha sheria hiyo amemteuwa Bi Fatma Idd Ali kuwa Naibu Mrajis wa Vizazi na Vifo. Uteuzi huo wote umeanza leo tarehe 14/1/2012

3 comments:

  1. Hongera zake!..pamoja na kwamba sielewi wasifu wake wa ndani, lakini kwa nje naonekana ana
    uwezo.

    Nilibahatika kumuona siku moja katika mdahalo juu ya mabadiliko ya katiba, na kwa kweli sio mimi tu niliefurahishwa na mchango wake bali hata wale wasiokua katika sisi walijiuliza kama keli Z'bar tuna wanasheria wazuri kiasi kile.

    Kila la kheri katika nafasi yake mpya.

    ReplyDelete
  2. huyu bwana na mimi nilimuona katika mchakato wa mustakbal wa katiba mpya pale taasisi, kwa kweli hoja zake ndio zimenishawishi kuhisi kua uwezo anao wa hii nafasi. hongera ibrahim

    ReplyDelete
  3. Ibrahim mzee ibrahim yuko vzuri

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.