Ni Grand Malt Kuidhamini kwa Miaka mitatu
Na Abdi Shamnah
VILABU
vinavyoshiriki ligi kuu ya Zanzibar, vimetakuwa kusimamia na kuweka mbele suala
la nidhamu, sambamba na kuepuka malumbano na migogoro isio na tija katika soka.
Changamoto jhiyo
imetolewa jana na Waziri wa Habari, utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali
Mbarouk katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani katika hafla ya uzinduzi wa Udhamini
wa Ligi kuu ya Zanzibar, itakayojuilikana kwa jina la ‘Grand Malt Premier
League’.
Kampuni ya
Kinywaji baridi kisicho na kilevi cha Grand Malt, imedhamini Ligi kuu ya
Zanzibar, kwa mkataba wa miaka mitatu kwa gharama ya shilingi Milioni 140,
ukijikita katika suala la utoaji huduma katika nyanja za usafiri, malazi,
chakula na zawadi kwa klabu zitakazoshiriki ligi hiyo.
Akizungumza na katika hafla hiyo iliowashirikisha viongzoi wa Wizara ya
Habari,Utamaduni,Utalii na Michezo,BTMZ, ZFA na wale wa klabu za soka, Waziri
Mbarouk, alisema nidhamu ni nyenzo muhimu katika uendelezaji wa soka, kwa
kuzingatia kuwa hakuna mdhamini atakaefurahia kudhamini ligi ambayo daima
inakabiliwa na migogoro.
Alisema njia pekee
ya kuwatia moyo wadhamini hao pamoja na wengine wenye azma ya kuidhamini ligi
hiyo ni kudumisha nidhamu na kuepuka migogoro.
Alisema Wizara
yake na Serikali kwa jumla itatoa kila aina ya ushirikiano katika kufanikisha
mchakato ulioanza wenye lengo la kulikomboa soka la Zanzibar kufikia katika
maendeleo.
Aidha aliliagiza
BTMZ kuweka utaratibu madhubuti kuona fedha zinazotolewa na wadhamini hao zinatumika
kama zilivyokusudiwa.
Katika hatua
nyingine Mbarouk alisisitiza msimamo wa Serikali na wananchi kuwa kwa mujibu wa silka na utamaduni wa watu wake,
vinywaji vya pombe havitaruhusiwa kudhamini michezo hapa nchini.
“Najua kuna
kampuni nyingi zilikuwa na hamu kuona wanakuwa wadhamini wa michezo hapa
Zanzibar kupitia pombe wanazotengeneza , hilo ni muhali na haliwezekani’,
alisema.
Alisema kampuni
zinazotenegenza vinywaji visivyo na kilevi kama ilivyo Grand Malt vinaruhusiwa
na vinakaribishwa kwa mikono miwili kudhamini katika aina za michezo tofauti.
Alimpongeza Waziri
Jihad (aliekuwa Waziri wa Wizara hiyo kabla yake) kwa juhudi kubwa alioifanya
hadi kukamilika kwa mchakato wa kumpata mdhamini huyo.
Mapema Meneja
Masoko wa Grand Malt, Fimbo Mohammed, alisema kuwa mkataba huo unaoanza Augost,
mwaka huu ukiwa ni asilimia 70 ya mahitaji ya bajeti yote, hivyo kutoa fursa
kwa wadhamini wengine kuweza kumalizia asilimia 30 zilizobaki.
Alifafanua kuwa
mkataba huo, utakuwa ukifanyiwa mapitio kila mwaka, na kutoa uwezekano wa fedha
hizo kuongezeka kutegemea na ufanisi utakaopatikana.
Aliwataka wadau wa
soka kushirikiana pamoja ili kuhakiksha mabadiliko ya kweli katika soka
yanafikiwa.
Alisema Kampuni
yake inaona fahari na heshima kubwa kudhamini ligi hiyo, na kuzitaka kampuni
nyengine kujitokeza ili kuleta mapinduzi ya kweli katika soka la Zanzibar.
No comments:
Post a Comment