Mbunge Konde, asaidia huduma za jamii
Na Hamad Shapandu, Pemba
JIMBO la Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, limekabidhiwa shilingi milioni 9 kwa ajili ya kununulia vifaa mbalimbali vya jimbo hilo kwa ajili ya kuimarisha huduma za kijamii.
Vifaa vilivyokusudiwa kununuliwa ni pamoja na pakti 50 za saruji kwa ajili ya masjidi-Mijahidia, (25) katika madrasa ya Tahfatul-Islam (15) za Masjidi mpya Mnarani (10) Madrasat al’shabab, pamoja na bati za kuelekea kwa ajili ya madarasatul Islamiya Konde na– Hidayatual-Islamiya
ya Vilima vitatu.
Akikabidhi fedha hizo, Mbunge wa jimbo la Konde, Khatib Said Haji, aliwataka wananchi wa vijiji mbalimbali vya jimbo hilo, kuzitumia fedha hizo vizuri kwa kununua vifaa vilivyokusudiwa.
Mbali na vifaa vilivyotajwa awali lakini Mbunge huyo alitaka kununuliwa saruji , bati , nondo , plaudi na mipira ya kusambaza maji.
Alisema katika kipindi cha miaka 5 ya Uongozi wake amekusudia kuchukua juhudi za maksudi kupunguza kero za wananchi kwa kuyapatia ufumbuzi matatizo yaliyo ndani ya uwezo wake.
“Kero na changamoto zilizopo katika jimbo langu zinaweza kuondoka kabisa iwapo fimbo ya umoja itatumika katika kuchochea kasi ya maendeleo”, alisema mbunge huyo.
Alifahamisha kuwa vifaa hivyo vitawanufaisha wanajamii na wanafunzi iwapo vitatumika vizuri na kwamba anaamini vitachukua muda mrefu ikiwa vitatunzwa vizuri.
Katika mikutano ya makabidhiano iliyofanyika katika kijii cha Konde , Kiungani , Kiumbemzito , Mijileni na vilima vitatu na kuhudhuriwa na madiwani , wajumbe wa kamati tendaji , Mjumbe wa BLW mstaafu.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenziwe, Omar Abdalla Is-haka wa Vilima vitatu Konde pamoja na kupongeza juhudi za Mbunge huyo alisema kitendo cha kutekeleza ahadi alizoziweka zimeleta imani kubwa kwao katika kuwaondolea shida watoto wao na uaminifu.
Nae, Diwani wa Jimbo hilo, Naima Nassor Khamis, alimpongeza katika kutekeleza ahadi pamoja na ushirikiano na kuwa wanaamini baada ya miaka mitano ya uongozi wake katika kuimarisha huduma za kijamii.
Hongera kwa kuanza kuutumia mfuko wa Jimbo kwa kuanza kujijenga kisiasa, inatia moyo maana hata baadhi ya wabunge wenzako kisiwani Pemba wanashindwa walau kuutumia huo mfuko kwa maslahi ya majimbo yao.
ReplyDelete