Na Mwanatanga Ame
WAZIRI asiyekuwa na wizara
Maalum, Mansour Yussuf Himid, amesema serikali tayari imeanza kuwahoji viongozi
wa serikali ambao wametajwa katika ripoti ya kamati teule ya Baraza la
Wawakilishi.
Kauli ya waziri huyo
ilikuja baada ya wajumbe wengi Baraza la Wawakilishi kuishutumu bajeti ya
serikali ya mwaka 2012/2013 kwa kudai ni kwanini serikali iko kimya kwa
kushindwa kuwachukulia hatua watu waliotajwa katika ripoti hiyo.
Alisema sio kweli kama serikali iko kimya kuifanyia kazi ripoti hiyo kwani
tayari wapo viongozi waliotajwa kuhusika na wizi unaodaiwa kufanyika katika
taasisi mbali mbali za serikali.
Alisema serikali
ilikubali kuunda kamati teule kwa kutambua suala hilo linafanyika kwa taratibu za kisheria
baada ya kuamuliwa na chombo hicho na kuwekewa muongozo wa kuifanya kazi hiyo.
Alisema haiwezekani
suala saerikali ikatoa maamuzi ya jazba kwani viongozi waliotajwa nao hawana
haki ya kusikilizwa na ni lazima kwa serikali yenye kufuata misingi ya kisheria
kuwapa haki ya kusikilizwa.
Alisema si vyema kunyosheana
vidole na waipe nafasi serikali kuifanyia kazi ili kuweza kuleta majibu sahihi juu ya suala hilo .
Akizungumzia juu ya
suala la yeye kutajwa kuhusika katika kundi la Jumuiya ya Uamsho, alisema hahusiki
nalo na hakubaliani na vitendo vya vurugu wanavyofanya.
Alisema vurugu
zinazofanywa na Jumuiya ya Uamusho yeye hakubaliani nazo kwa vile haungi mkono
kwa Wazanzibari kurudi katika visa vya uhasama vilivyowahi kutokea hapa nchini.
Akiendelea alisema
jambo linalohitajika kufanywa ni kuona kunajengwa uvumilivu kwa kuwaelekeza
zaidi wananchi nini cha kufanya na sio kuandaliwa mazingira ya kupambana na
wanaotoa kauli za kuukataa Muungano.
Aidha, Mwakilishi
huyo alisema bajeti iliyoiandaa serikali ni vyema wajumbe wa Baraza hilo wakaikubali kwani
bajeti iliyopita imeonekana kupata mafanikio mbali mbali.
Alisema suala la
kuongeza kodi lililofanyika kwa Zanzibar
bado hazilingani na kodi za bajeti za ukanda wa Afrika Mashariki lakini serikali
imeanza kuwa na bajeti inayojitegemea kwa baadhi ya huduma.
Alisema hatua hiyo
ni jambo la faraja kwa serikali ya Zanzibar na
ni vyema kwa Wajumbe wa baraza hilo wakaliunga
mkono suala hilo .
Alisema serikali kwa
kiasi kikubwa imesaidia kuona misamaha ya kodi kwa mwaka huu imeweza kuokowa
bilioni 9 jambo ambalo ni tofauti na miaka iliyopita.
No comments:
Post a Comment