Habari za Punde

Balozi Seif Ali Iddi Mgeni Rasmi Mashindano ya Kuhifadhi Qur-an Al-Haramain Mjini Dar es salaam

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa nasaha zake mara baada ya kushuhudia mashindano ya kuhifadhi Quran yaliyoshirikisha Wanafunzi kutoka vyuo mbali mbali vya Bara na Zanzibar. Kulia ya Balozi ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Ali Muhidini.

 Jopo zima la Majaji wanaoendesha mashindano ya Kuhifadhi Quran katika chuo cha Kiislam cha Al Haramain Mjini Dar es salaam wakiendelea na upembuzi wa kupata washindi katika mashindano hayo.

Mwanafunzi Rashid Seif Hamad kutoka Chake chake Pemba  akiwa katika meza ya mashindano ya kuhifadhi Quran hapo chuo cha Kiislamu cha Al Haramain Mjini Dar es salaamu akionyesha umahiri wake. Rashid  ameibuka msindi wa pili katika kuhifadhi Juzuu 30.
Mwakilishi wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Iran Nchini Tanzania Sheikh Murtaza akimkabidhi Mgeni rasmi Balozi Seif zawadi ya Quran iliyohifadhiwa katika mfumo wa kisasa wa Digital hapo katika mashinda ya kuhifadhi Quran Al Haramain Mjini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Wanawake wa Kiislamu Tanzania { Bakwata } Ukti Shamim Khan.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi zawadi ya Baskeli Mwanafunzi Khalifa Ali Faki baada ya kupata ushindi wa Pili wa Juzuu 3 kwenye kilele cha mashindano ya kuhifadhi Quran.Kulia ni Mwenyekiti wa Waislamu wanawake Tanzania { Bakwata } Ukti Shamin Khan.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi mshindi wa kwanza wa mashindano ya kuhifadhi Quran Juzuu 30 Mwanafunzi Abdullhamid Masoud Laptop na Printer katika mashindano hayo yaliyofanyika viwanja vya chuo cha Kiislamu cha Al Haramain Jijini Dar es salaam.Mwanafunzi Abdullhamid na wenzake mshindi wa pili na tatu pia wamefunguliwa akaunti ya shilingi 1,000,000/- kila mmoja na Benki ya Amana Mjini Dar es salaam.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa kamati ya mashindano ya kuhifadhi Quran, Majaji pamoja na Uongozi wa Bakita ukiongozwa na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Ali Muhidini Mgogoni.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.