Habari za Punde

Wakaazi wa Kidagoni, Kidoti wapatiwa misaada

 Wanafunzi wa Skuli ya Kidagoni Mkoa wa Kaskazini Wadi ya Kidoti wakiwa katika Banda lao la Skuli ambalo wakisomea Kabla ya Serikali kuwajengea Jengo jipya la Skuli hio(lililo upande wa kulia)kiji hicho kinakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa pamoja na Barabara ya kufikia huko,Maji safi na salama na Kituo cha Afya.
 Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Ofisi ya Zanzibar Mcha Hassan Mcha(kulia) akitoa hotuba ndogo baada ya kukabidhi Msaada wa Vifaa mbalimbali vya Skuli ya Kidagoni na kuahidi kuwafikishia Maji safi Skulini hapo.Kulia yake ni Kamishna wa Elimu Zanzibar Maryam Abdalla Yussuf.
-Kamishna wa Elimu Zanzibar Maryam Abdalla Yussuf.akifafanua jambo wakati akitoa hotuba baada ya Kupokea Msaada wa Vifaa mbalimbali vya Skuli ya Kidagoni ilioko Mkoa wa Kaskazini Wadi ya Kidoti.kushoto yake ni Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Ofisi ya Zanzibar Mcha Hassan Mcha na kulia yake ni Afisa Utumishi Mwandamizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) Ofisi ya Zanzibar Haula Kassim.
 
Baadhi ya Wananchi wa Kjiji cha Kidagoni Wadi ya Kidoti wakisikiliza Hotuba ya Kamishna wa Elimu Zanzibar(hayupo pichani)katika sherehe za kukabidhiwa Vifaa mbalimbali vya Skuli ya Kidagoni.

PICHA NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.