Timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes leo hii imefungwa 2-0 na timu ya taifa ya Malawi katika mchezo wa mwisho wa kundi C katika mchezo uliopigwa katika uwanja wa Wankulukuku
Magoli ya Malawi yalifungwa mapema na Ndaziona Tchasalia dakika ya 3 na goli la pili lilifungwa na Chuikepo Msowoya katika dakika ya 6 ya mchezo huo.
Zanzibar heroes licha ya kujaribu kusawazisha ilijikuta ikikabiliana na ukuta mgumu wa timu ya Malawi ambayo pia imefanikiwa kuingia katika Robo fainali kwa kumaliza na pointi sita.
Zanzibar imeweza kufuzu robo fainali kutokana na kuwa "best loser" kwa kuweza kupata pointi nne katika mechi zake mbili za awali dhidi ya Eritrea na Rwanda.
Itapambana na Burundi siku ya Jumatatu saa 10.00 jioni katika mchezo unaotarajiwa kutoa upinzani mkali kwani Burundi haikupoteza hata mchezo mmoja katika kundi lake huku Zanzibar ikijaribu kukumbuka historia yake ya kuweza kulinyakua kombe la Cecafa mwaka 1995 katika nchi ya Uganda.
No comments:
Post a Comment