Joseph Ngilisho,Arusha
ASKOFU wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)
Dayosisi ya Kaskazini kati,marehemu Askofu Dk. Thomas Laizer atazikwa siku ya
Ijumaa katika kanisa kuu la KKKT.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamati ya mazishi na familia ya marehemu, iimeeleza kuwa marehemu
atazikwa katika kanisa hilo
lililopo mjini kati Arusha,kama ishara
ya kuwaenzi maaskofu wa
kanisa hilo ,tofauti na awali ambapo taarifa zilidai
angezikwa nyumbani kwake.
Aidha taarifa hiyo imesema kuwa waumini na washirika wa kanisa
kuu na makanisa yote ya KKKT nchini, wananchi, ndugu jamaa na marafiki
watapata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa marehemu kuanzia siku ya
Alhamisi mchana.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa mwili wa Askofu Laizer
utalala kanisani hapo hadi Ijumaa kwa mazishi.
Marehemu Askofu Laizer aliyezaliwa Machi 10, 1945 katika
kijiji cha Kitumbeine wilayani Longido
na baade kupata elimu yake ya msingi hadi darasa la nane Longido na
kumaliza mwaka 1965.
Askofu Laizer, aliendelea na masomo yake ya juu ndani na
baade kujiunga na masomo ya Theolojia katika chuo cha Makumira na baade kuongeza
masomo nchini Marekani.
Marehemu wakati wa uhai wake alikuwa Mwinjilisti na mchungaji
katika makinisa mbalimbali nchini na baade kuwa Mkuu wa jimbo na Mkuu wa Sinodi
na baade kuwa Rais wa Sinodi kabla ya kupandishwa cheo kuwa Askofu wa kwanza wa
Dayosisi ya Arusha ambayo kwa sasa ni Dayosisi ya Kaskazini Kati.
Mazishi ya Askofu Laizer yanatarajiwa kuhudhuriwa na
idadi kubwa ya watu kutoka maeneo mbalimbali nje na ndani ya nchi, huku viongozi
wa serikali wakitarajiwa kuongoza mazishi hayo.
No comments:
Post a Comment