Habari za Punde

Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho akitoka katika Ukumbi wa Baraza baada ya kuahirisha Kikao cha asubuhi, kwa ajili ya mapumziko na kurudi jioni kuendelea na kuchangia miswada iliowakilisha katika Kikao hicho.  
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, akibadilisha mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha Omar Yussuf Mzee, wakitoka ukumbi wa mkutano baada ya kuahirishwa kikao cha asubuhi.
 Mwakilishi wa Donge na Waziri wa Ardhi Maji Nishati na Makaazi Juma Ali Shamuhuna, akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Ferej,  
 Wajumbe wakibadilisha mawazo nje ya Ukumbi wa Baraza.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Maji Nishati na Makaazi Mustafa Aboud Jumbe akizungumza na Wajumbe wa Baraza baada ya kikao cha asubuhi kuahirishwa wakiwa katika viwanja vya Baraza, kushoto Mwanasheria wa Mkuu Zanzibar Othman Masoud na Mwakilishi wa MjiMkongwe Ismail Jussa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Mwakilishi wa Dimani Dk. Mwinyihaji Makame na Mwakilishi wa Bububu kulia Hussein Ibrahim Makungu (BHAA) wakitoka katika ukumbi wa baraza baada ya kuahirrishwa kwa kikoa cha asubuhi cha maswali na majibu na kujadili mswada wa Sheria ya Uundwaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati. Zanzibar

1 comment:

  1. haya mambo ya kijahili bado tunayo tu , kwa kuwa tumerithi , kuna haja gani kwa spika kuja na eskoti na rungu na mtu mbele na nyuma , inaashiria nini? hebu nielimisheni, mimi naona ni upumbavu tu wala si ujinga. Miaka ya zamani hilo rungu lilikuwa kutishia wachangiaji wasivuke mipaka , lakini kama tunaamini demokrasia , kuna haja gani ya rungu? tumesema watu wote ni sawa na wanastahili heshima, sasa kuna umuhimu gani wa wengine kupewa heshima za uungu? halafu bado Nd.Kificho una sijda kubwa na kusali sali , jee hivi unavyofanyiwa unakubali ni sawa? hapakuwa na kiumbe aliye bora katika ulimwengu kama nabii (saw) , lakini alipoona watu wanamsimamia akipita au akiwatokea , aliwakataza , jee hufikiri? au unafikiri hizi ni riwaya za kupass taim? na kufurahisha baraza? kuna mafunzo kwa wenye kuelewa , usije kusema hukukumbushwa, umri wako uko karibu na Mungu kuliko na dunia , jioshe kabla ya kuoshwa , asie sikia la mkuu.......

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.