Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi

 Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar Suza kilichokuwepo Tunguu wakiwa katika Ukumbi wa Juu wa Baraza la Wawakilishi wakifuatilia maswali na majibu pamoja na mijadala mbalimbali inayoendelea katika Baraza hilo lililokuwepo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
 
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohd Aboud Mohd akijibu Maswali mbalimbali aliyoulizwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi lililokuwepo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
 Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni Mbarouk Wadi Mussa kulia akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Baraza kupitia nafasi za Wanawake Mgeni Hassan Juma wakipitia karatasi mbalimbali za maswali na majibu katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  lililokuwepo Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
 
Waziri wa Katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakari akionyesha karatasi ya Warka wa Kiwanja alipokuwa akijibu maswali mbalimbali aliyoulizwa na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi huko Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
 
PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR

10 comments:

  1. Hao mabinti wa SUZA usiowaone hivyo, ukadhani wanafkiria mambo ya maana.

    Hapo wanachofkiria ni mshahara wa ualimu, kununua madira, kuolewa na kuzaa watoto bila ya utaratibu.

    Na kama hao wenye 'rangi rangi' ndio kabisa, anaweza kutokea 'mbeba boxi' au mmanga mbovu akasema apelekewe ukawa ndio mwisho wa elimu yake.

    Kwanza, kuwa hawana uwezo wa ku'challenge' mwanamme hata kama hakusoma hata darasa moja.

    Wakati kuelimisha 'mtoto wa kike' kwenye jamii nyingine ni kuelimisha jamii yote, paha kwetu tofauti, badala yake ni kuharibu pesa...hawabadiliki!

    ReplyDelete
  2. Hawa mabinti wa SUZA hawafikirii lolote isipokua kupata kazi, kununua 'madira', kuolewa na kuzaa bila ya mpangilio.

    Z'bar watu hawabadiliki hujui aliyesoma wala asiesoma'naona vyangu naona tuu'

    ReplyDelete
  3. Jamii yetu hapa zbar, doa, huona kitu cha maana ,bila ya kujali muoaji au muolewa, swali la elimu tumepiga kele sikunyingi .Elimu inayopendwe kujifunika,nyuso na kuvaa mabaibui,ya kubana kujisifia kaolewa maranyingi elimu ya kupata ajira hawaitaki wanasema wao wameumbwa wajeolewatu

    ReplyDelete
  4. mmmh si kweli haya maneno mengine, tusisahau kuna kitu kinaitwa mgawanyo wa kazi ,kwa mfano unapoenda ofisini mwalimu mkuu , walimu wengine , msafishaji shule , mlinzi wa shule , tarishi wa ofisi , hawa wote wana umuhimu wao , haiwezekani wote wakawa walimu , wala haiwezekani wote wakawa wasafishaji , lazima kuwe na uwiano ili kazi zifanyike. Kwa hio mwanamke ana nafasi nyingi katika jamii, kuzaa na kulea na kuangalia nyumba na mali ya mumewe ni kazi vile vile usifikiri rahisi , hebu jaribu kuchukua jiwe la kilo mbili tu ulifunge tumboni utembee nalo kwa wiki moja halafu useme, kama tusingezaa wewe usingekuwepo sasa hivh kubwabwaja maneno ya kifedhuli. Kusoma ni kuondoa ujinga kama kuajiriwa au laa ni hiari , mnataka tuje maofisini mtuajiri halafu muanze kutunyanyasa tu,

    ReplyDelete
  5. Mtoa maoni wa kwanza na wa pili hapo ndio mwisho wenu wa kufikiri?
    Hebu nendeni mkasome mafundisho ya Mtume (S.A.W)kuhusu wanawake mutapata kujuwa, kama ni waislam munajuwa kama kilichofundishwa na Mtume (S.A.W)ndio uongofu.

    ReplyDelete
  6. Katika dunia ya sasa kuzaa tu nakulea watoto hakusaidikitu, aowanaokaba na kuvuta unga pia wamezaliwa,katika hayo makuzi mazuri, wanayo tuambia muamsho malezi mazuri hupatikana kwa kufuata shari, sasa tuna taka wasome elimu ya kidunia ili wawe,madaktari, wana sheri, mainjinia na fani nyengine, tuone kama watazalilsha maofisini ikiwa wana fani hizo

    ReplyDelete
  7. Mchango wa wanawake ktk jamii sote tunaulewa kwani tumezaliwa na tumelelewa na wanawake.

    Pia tumeowa na tuna ndugu na dada zetu lkn. tunalozungumzia hapa ni suala la elimu na wanawake.

    Nasistiza mchango wa elimu kwa wanawake wa Z'bar ni mdogo sana, wanashindwa kuitumia ipasavyo!

    Anonymous wa nne amenisikitisha sana kuutumia UISLAMU kufichia ujinga. hii sio sahihi.

    Imekua ni kawaida Z'bar ukilaumu: W'wake kwa kutokuitumia elimu vizuri mtu atakwambia "sisi waislamu" uongozi mbaya"sisi waislamu"...jamani kweli uislamu ni hivyo?

    Mafundisho ya mtume yamo ktk khadithi tofauti tofauti naomba unitajie kitabu kimoja wapo ili nikajisomee!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama mchango wa wanawake unaeleweka kwanini munalaumu?

      Inaonekana watu wengine wanaona mwanamke akienda shule basi ni lazima awe katika ajira vyenginevyo atakuwa hana mchango katika jamii. Hii ni dhana potofu na haina ukweli.Tufahamu inaanza family ndio tukapata jamii na kuendelea juu Taifa na mengineyo.

      Mwanamke mwenye elimu atakuwa na uwezo mzuri wa kushughulikia familia yake kwa maana hiyo patakuwa na shina zuri la hiyo jamii yenyewe.UISLAMU unaelezea mfumo mzima wa maisha ndiyo maana inakuwa ndio point of REFERENCE(nawala sio pa kufichia UJINGA kama ulivyosema)

      Nenda kwenye kitabu kinachoitwa RIYADHUL-SWALIHIIN.

      Delete
  8. Njia moja ya uongofu ni kusoma na kutafuta ajira ili upate riziki halali, kama uislam ulivyo sema, sisi hapa petu tunakazania kuwaoza watoto waislam, nafasi za ajira zipo tele kwa wanawake wenye taaluma, hapa ,zbar, ukienda mkoa wa kaskazin mahoteli yameja, na chuo kipo maruhubi, mbona hatu wahimzi kwenda kusoma, tuna waachia watanganyika, tunataka kupumua haliyakua vipofu

    ReplyDelete
  9. Mwandishi tengeneza kiswahili, blog hii inasomwa na wengi. Naona sio sahihi kuandika "kilichokuwepo tunguu". this is past tense. Sahihi ni "kilichopo"

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.