Habari za Punde

Ujenzi Kinyume na Sheria za Ujenzi Hiyooooo

 Afisa wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA akionesha sehemu ilipopita bomba la maji safi kwa  kutowa huduma kwa Wananchi wa maeneo ya Mbuyu Mnene sehemu ya bomba hilo limejengwa ukuta wa nyumba ya mkaazi wa maeneo hayo na kuwakosesha wezake huduma hiyo, ikizingatiwa  katika kipindi hichi kuelekea katika mwezi wa Ramadhani huduma ya maji hutumika kwa wingi katika kipindi hicho.  
 Mwananchi wa mtaa wa Mbuyu Mnene Bakari Abeid, akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Abdalla Mwinyi Khamis mwenye kufia akiwa namaofisa wa ZAWA, ukuta uliopita juu ya bomba la maji na kuwafanya wao kukosa huduma hiyo. 
Ofisa Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA Zahoro, akizungumza na Wananchi wa maeneo ya Mbuyu Mnene waliofika katika Ofisi za ZAWA kumlalamikia Mwananchi wa mtaa huo kujenga ukuta juu ya bomba la maji safi na kushindwa kutowa huduma kwa wananchi wa mtaa wa pili kwa kulibana bomba hilo kushindwa kupitisha maji na kuwafanya kuwa katika hali ngumu ya kupata huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.