Na Pascal
Buyaga, MUSOMA
CHAMA
cha NCCR Mageuzi kimesema hakikubaliani
na hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, aliyoitoa Dodoma wakati akizundua bunge
maalum la katiba, kikisema hotuba hiyo imeligawa taifa.
Kauli
hiyo imetolewa mjini Musoma na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Leticia Ghati
Mosore, wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema
rais alipaswa kuzindua na kisha kuwaachia
wajumbe waamue kile kilichowasilishwa na Tume ambayo aliiunda yeye, badala
ya kupingana na tume hiyo.
Alisema
kama anafikiria Tume haikufanya kazi vya kutosha, alipaswa aaite na kuwashauri
wajumbe wake kabla ya kuiwasilisha.
“Tulisikitika kumuona Rais
anatoa mapendekezo ya chama chake, wakati yeye ni alama ya taifa, kwa
nini alikubali kupokea rasimu ya kwanza na rasimu ya pili wakati anajua ilikuwa na makosa kwa nini asingeshauriana na tume hiyo ambayo imepoteza mabilioni ya walipa kodi ya
Watanzania,” alihoji.
Aidha
alisema hotuba ya Kikwete imezungumzia kero za
upande mmoja wa Zanzibar
badala ya kuzungumzia keri za muungano.
“Sisi
kama Watanzania tunamuomba Mungu awape busara wajumbe wa bunge la katiba,
lakini kama NCCR-Mageuzi tunapinga hotuba yake,” alisema.
Kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa, alisema chama
chake kimejipanga kuhakikisha kinachukua idadi kubwa ya mitaa.
No comments:
Post a Comment