Na
Mwandishi wetu
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete, amewataka wakazi wa
Handeni na maeneo inakopita barabara ya Mkata–Handeni na Korogwe–Handeni,
kutumia ipasavyo fursa ya barabara hizo,kuboresha maisha yao .
Alitoa
rai hiyo wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara inayounganisha makao makuu ya wilaya ya
Handeni na barabara kuu ya Tanga-Dar es Salaam kupitia Mkata na upande mwingine
kuunganisha na barabara kuu ya Tanga-Moshi- Arusha kwa upande wa Korogwe.
Alisema
lengo la serikali ni kuona barabara ya Mkata hadi Handeni inaendelezwa hadi
Kondoa kupitia Kiberashi kwani kufunguka kwa ukanda huo kutakuwa chachu ya
kuinua uchumi.
Akiwasilisha
tarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania
(TANROADS), Eng. Patrick Mfugale, alisema barabara ya Mkata - Handeni ambayo imejengwa
kwa kiwango cha lami ina urefu wa kilometa 53.2 na imejengwa na Mkandarasi
Sinohydro Corporation Ltd kutoka Jamhuri ya Watu wa China kwa gharama ya shilingi
bilioni 57.3.
Alisema
mkataba wa mradi huo ulisainiwa mwezi Juni 2009 na kazi zikakamilika Novemba
2012 baada kutatua changamoto zilizokwamisha kukamilika kwa mradi huo mapema.
Ufunguzi
wa barabara hiyo umeenda sambamba na ufunguzi wa barabara ya Korogwe hadi Handeni
ambayo imekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Akitoa
tarifa kuhusu miradi huo wa Korogwe- Handeni, Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Eng.
Patrick Mfugale, alisema mkandarasi Sinohydro Corporation Ltd ndiye pia
iliyejenga barabara hiyo ambayo ina urefu wa kilometa 65.
Naye
Waziri wa Ujenzi,Dk. John Pombe Magufuli, akielezea baadhi ya faida
zitakazopatikana kutokana na kujengwa kwa barabara hizo alibainisha kuwa
barabara ya kutokea Korogwe hadi Handeni ndiyo itakayosaidia kwa kiasi kikubwa
kupunguza msongamano wa gari katika barabara
kuu ya TANZAM hasa kwa wasafiri na wasafirishaji wanaotokea maeneo ya
Iringa, Mikumi na maeneo mengine ya ukanda huo.
No comments:
Post a Comment