Na Joseph
Ngilisho,ARUSHA
POLISI
mkoani hapa wamemuua kwa kumpiga risasi askari wa jeshi la kujenga taifa (JKT)
kikosi cha Oljoro na kumjeruhi mwingine katika mapambano yaliyotokea eneo la
kwa Mromboo,baada ya marehemu kudaiwa kumpokonya askari polisi magazine
iliyokuwa kwenye silaha aina ya SMG.
Marehemu
ametambulika kwa jina la Joram Mnyakule (24)mwenyeji wa Kigoma huku majeruhi
aliyelazwa katika hospitali ya Mkoa Mount Meru akiendelea kupatiwa
matibabu bado hajatambulika.
Kwa
mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,ambaye aliomba kutotajwa jina lake akihofia
usalama wake, tukio hilo limetokea juzi majira ya saa 4:00 usiku,katika eneo
hilo la kwa Morombo ,ambapo marehemu akiwa na wenzake 20 walivamia eneo hilo na
kutembeza kichapo kwa raia yeyote wanayekutana naye wakidai wanasaka sare
zao zilizoibiwa.
Hata
hivyo, polisi wa doria walipata taarifa kuhusiana na tukio hilo na kufika eneo
hilo,ambapo walianza kuwasihi wanajeshi kuacha vurugu lakini katika hali
isiyokuwa ya kawaida ,wanajeshi hao waliwageuzia kibao na kuanza kuwashambulika
huku baadhi yao
wakitaka hata kuwanyang'anya silaha.
Taarifa
zinadai kwamba polisi walipofika eneo hilo kwa lengo la kuzuia ghasia
zilizokuwa zikiendeshwa na watu hao wanaosadikiwa ni wanajeshi waliokuwa
wakimsaka kibaka anayedaiwa kukwapua mfuko uliokuwa na sare za mmoja wa
wanajeshi hao,ndipo wanajeshi hao walipowageuzia kibao polisi na kuanza
kuwashambulia.
Hali
hiyo ilichukua takribani dakika 20 wakivutana huku marehemu akichukua jukumu la
kunyang'anya mmoja wa askari polisi 'magazine' iliyokuwa kwenye silaha aina ya
SMG na kutaka kutokomea nayo,ndipo askari polisi mmoja alipomfyatulia risasi
mgongoni na kupoteza maisha na kumjeruhi mwingine.
Hali
hiyo ilisababisha wanajeshi wengine waliokuwa eneo hilo kuanza kutawanyika wakihofia usalama wao.
Kamanda
wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas alipotafutwa kuzunngumzia tukio tukio
hilo hakupatikana,hata hivyo baadhi ya polisi walioshuhudia walithibitisha na
kueleza kuwa taarifa zaidi zitatolewa na kamanda.
Mwili
wa marehemu umehifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya mkoa
ya Mount Meru kwa ajili ya uchunguzi.
No comments:
Post a Comment