Habari za Punde

Utafiti: Wanawake wengu wanafanya mapenzi kinyume cha maumbile

 Na Khamis Malik, WUUVWW
IMEELEZWA asilimia 25 ya wanawake wanafanya mapenzi kinyume cha maumbile ama na waume zao au na wanaume wengine kama njia ya kukimbia kupata ujauzito na mambo mengine.

Takwimu hizo zimetolewa na Katibu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar kutoka wilaya ya magharibi, Sheikh Nassor Hamad Omar, wakati akiwasilisha ripoti ya awali ya utafiti wa kamati ya kupambana na vitendo vya liwati katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Tunguu, kwenye kongamano la vijana kuhusu udhalilishaji wa kijinsia na mimba za mapema.

Alisema takwimu hizo zimekusanywa kutokana na utafiti uliofanywa na Jumuiya ya Maimamu (JUMAZA) katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.

Alisema sababu ya kufanya hivyo, ama wanawake hao wanaogopa kupata ujauzito hasa wale ambao bado hawajaolewa lakini wako kwenye mahusiano na hata wale walioko kwenye ndoa.


Aidha alisema utafiti huo umegundua watoto wengi wenye umri wa kuanzia miaka tisa hadi 20, wanaingizwa katika vitendo viovu ikiwemo liwati na usagaji.

Alizitaja sababu kubwa zinazopelekea kuenea kwa uovu huo kuwa ni pamoja na tamaa, matumizi mabaya ya utandawazi, imani za kishirikina kwa kupiga ngoma kama vile vibuki, kupenda kuiga tabia mbaya na watalii wakorofi.

Alisema  kutokana na tatizo hilo, kamati yake imefanya utafiti wa tatizo hilo na kutoa elimu kwa taasisi mbalimbali ambapo nyengine zimekubali kushirikiana nao bega kwa bega ili kuondoa tatizo hilo.

Alisema Jumuiya imeandaa kitabu ambacho kimeandikwa kwa kuzingatia zaidi misingi ya dini mbili za Kiislamu na Ukiristo.

Aidha, alisema wamefanikiwa kuvitembelea vyuo vya Quran na taasisi nyengine na kukutana na walimu, wanafunzi, wazazi na walezi ili kufikisha ujumbe na taarifa za utafiti huo.

Akizungumza kwa huzuni kubwa Shekhe huyo alisema inasikitisha kuona vijana wa kizanzibari wanafanya liwati huku wengine wakishangiria na kuchukua picha.

Nao vijana walioshiriki kongamano hilo, wakichangia ripoti hiyo, wamekiri kuwa vitendo vya liwati vipo na ni maarufu na vinafanywa  kwa wingi hata maeneo ya vijijini.

 “Vyombo vya habari vinapaswa kutumiwa kikamilifu kutambulisha na kutangaza uchafu huu unaotia doa jamii ya Kizanzibari na taifa letu” alisikika mmoja wa vijana hao akizungumza kwa masikitiko.

Washiriki hao walisema kuwa sheria zilizopo sasa zinatoa mwanya kwa wahusika kutotiwa hatiani na kutoa nafasi ya kuendelea kufanya makosa.

Walisema serikali kwa asilimia kubwa inapaswa kuwajibika na ni lazima iweke mikakati imara ya kutunga sheria ya kudhibiti suala hilo.

Aidha,  waliahidi kuvitumia vikundi vyao kuelimisha juu ya mapambano hayo na kwamba watazitumia maskani zao kulizungumzia tatizo hilo kwa uwazi.

Kongamano kama hilo linatarajiwa kuendelea katika mkoa wa mjini magharibi.

9 comments:

  1. Subhna-llah
    Zanzibar imekwisha ikiwa Wari Wanazini kama mvua.. enzi zetu weeee... Ulikua mtu huruhusiwi ata kutoka. Ukeshakuvunja ungo tu mchezo na watoto wanaume ulikua mwiko.... Subutu... Sikuhizi Mitoto ya Kibara imejaa na wenetu wa Kiume nao wakeshakupata balekhe na wakiona wanawake wameviringa ..Huwa hawasikii hawaoni..

    Kwanini serikali isichukue hatua yakukomesha Zinaa... Na Maradhi hayo yaliojaa ndio maana HIV imezidi Zanzibar.

    ReplyDelete
  2. Taireni,hakuna utafiti wa aina hiyo,vilitumika vigezo gani au criteria zipi kuligundua hilo.Kama yanafanyika hayo ni ndani watafiti walikuwa wapi.Huaje mke na mume watoe taarifa kama hizo.Inakuwaje wanawari watoe jambo kama hilo. Tunahitaji maelezo kwa mapana.Hivi yawezekana mke na mume iwe walifanye tendo hilo na baadae wakubali kupigwa picha na wengine washangirie? Jamani punguzeni kuzuwa.

    ReplyDelete
  3. hapa kuna namna inapikwa ili kufanya vidonge na dawa za majira zipate nguvu ya kuuzwa kwa kisingizio cha kuzuia haya mambo ambayo wala hayako, hakuna jengine , nakubaliana na anonymus no 2 walifanya vipi huu utafiti? wanafiki watakuwa katika tabaka ya chini ya moto , enyi mnaojiita JUMAZA kweli mnamwogopa mungu?

    ReplyDelete
  4. Mimi Napatwa na shaka ya uhakika wa na chanzo cha hiyo asilimia iliyoelezwa katika ripoti hiyi, sikatai katika jamii ni kweli vitendo hivyo vipo lakini si kwa kiasi kama kilicholezwa, huo unaoelezwa ni utafiti hauoneshi namna ya takwimu husika zilivyopatikana kama vile idadi ya walioulizwa maswali, umri wao, jinsia yao na maeneo gani na gani utafiti huu ulifanyika na hata njia zilizotumika kama vile madodoso gani yalitumika kukusanyia hizi taarifa,si vyema kuandikwa takwimu zilizobuniwa kwani matokeo yake ni kuharibu taswira ya jamii, ni kweli vitendo hivi vipo jamii na serikali inatakiwa kuchukua hatua visiendelee kukua na kuharibu kizazi chetu, lakini napingana na usahihi wa matokeo ya unaoitwa huo utafiti.

    ReplyDelete
  5. Kiukweli hili jambo lipo na halitaki utafiti na mkitaka ukweli nendeni labour hospital mtayapata! najuwa hata ikija maelezo ya vyanzo vya kuongezeka mabaradhul (makaka powa)i Zanzibar pia mtapinga kuwa hakuna mabaradhuli Zbar! that is our culture to hide the reality !Labda aseme politician ndio mtaungamkono ! That is zanzibares, that is the way we are!

    ReplyDelete
  6. hee mshawaita masheikh wanafik? mshawakebehi ! mshawazarau ! Je itakuwaje ikiwa wao walitoa kabisa methodology na modality waliotumia mpaka wakapata scientific data ila mwandishi hakuwa na uwezo au nafasi ya ku "quote" vizuri na kuandika, bora vizuri tungeuliza kabla ya kubeza. Pengine ungekuwa unamjua huyo sheikh Nassor Hamad Omar usingeweza hata kuandika. Au ndo mshazoea kubeza kazi za masheikh?

    ReplyDelete
  7. hivi nyie anonymous hamuamini hayo yalotafitiwa?hadi watoto wenu au wa jamaa zenu wawe waathirika wa tatizo hili?
    amini usiamini,tatizo lipo!
    kama tutashindwa kuamini utafiti tukachukuwa hatua,tunakuwa sehemu ya tatizo.

    ReplyDelete
  8. Tunaomba ripoti kamili ya utafiti ichapishe ndugu mwandishi ili tujue huu utafiti ulifanyika vipi?

    ReplyDelete
  9. Good
    Huwa nayasikia sana
    Lkn mkiandika muandike n ushahidi n vyanzo ili wasomaji wajiridhishe n pasiwe n mkanganyo
    Elimu ukiificha faida yake n kukuza ujinga n maovu t

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.