Habari za Punde

Rais awapongeza Wafanyakazi Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,(kushoto) Katibu Mkuu Kiongozi Dkt.Abulhamid Yahya Mzee,(kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Makame Mwadini (wapili kulia) wakiwapongeza wafanyakazi mbali mbali wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika hafla ya chakula iliyofanyika  baada ya kupitishwa bajeti za Wizara hizo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi,hafla hiyo ilifanyika leo viwanja vya Ikulu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wafanyakazi wa Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi baada ya kula nao pamoja chakula katika fahla ya kuwapongeza wafanyakazi hao baada ya  kupitishwa bajeti za Wizara hizo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea ,hafla hiyo ilifanyika leo viwanja vya Ikulu,(wapili kulia)Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi,akifuatiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Haji Omar Kheri.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara mbali mbali  zilizo chini ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wakiwa katika  hafla ya chakula iliyofanyika  baada ya kupitishwa bajeti za Wizara hizo katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea ,hafla hiyo ilifanyika leo viwanja vya Ikulu
  Baadhi ya watendaji na washauri wa Ofisi ya Rais Ikulu  wakiwa katika  hafla ya chakula iliyofanyika  baada ya kupitishwa bajeti za Wizara zilizo chini ya Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi katika kikao cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea ,hafla hiyo ilifanyika leo viwanja vya Ikulu(Ramadhan. Othman Ikulu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.