STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 6.12.2014

MAREKANI imezipongeza juhudi zinazochukuliwa na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein katika kuiongoza Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa ambayo imepata mafanikio makubwa.
Balozi wa Umoja
wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe.
Amina Salum Ali, aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein Ikulu mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo
hayo, Balozi huyo wa AU nchini Marekani alisema kuwa mafanikio yaliopatikana
ndani ya miaka minne ya uongozi wa Dk. Shein ni makubwa na yana kila sababu ya
kupongezwa kutokana na juhudi anazozichukua katika kuisimamia na kuiongoza
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa.
Alisema kuwa
Marekani inazipongeza juhudi hizo sambamba na uongozi wa Dk. Shein kwa
kuendelea kusimamia amani na utulivu hapa nchini.
Balozi huyo wa AU
nchini Marekani alieleza kuwa mafanikio hayo yote yamepatikana kutokana na
uongozi imara wa Dk. Shein ambao unaenda sambamba na busara zake hekima na kujali
wananchi anaowaongoza. Pia, Balozi huyo alipongeza mafanikio yaliofikiwa katika
kuimarisha uchumi wa Zanzibar pamoja na mikakati iliyowekwa katika uimarishaji wake.
Aidha, Balozi
Amina alieleza kuwa Zanzibar imeweza kujijengea sifa kubwa ndani na nje ya nchi
na kuwa kigezo kwa nchi za Bara la Afrika ambazo zinaongozwa na mfumo wa
Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Nae, Dk. Shein
kwa upande wake alieleza kuwa Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa imeweza kupata
mafanikio makubwa hapa nchini.
Alisema kuwa
kuwepo kwa Serikali hiyo kumeweza kuwaweka viongozi wa vyama vya siasa pamoja
na kuweza kujalidi masuala mbali mbali ya nchi kwa mashirikiano ya pamoja bila
ya kujali itikadi zao za kisiasa.
Dk. Shein alisema
kuwa ndani ya miaka minne ya uongozi wake chini ya Serikali hiyo mafanikio makubwa
yameweza kupatikana huku akisisitiza kuwa siasa ni maendeleo na kustahamiliana
na si vyenginevyo.
Aidha, Dk. Shein
alitumia fursa hiyo kutoa shukurani na pongezi kwa Marekani kutokana na juhudi
zake za kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika masuala mbali mbali ikiwa ni
pamoja na kuimarisha na kuendeleza miradi ya maendeleo.
Wakati huo huo, Dk. Shein alikutana na Balozi Mdogo wa Msumbiji anayefanya kazi zake Zanzibar Mhe. Jorge
Augusto Menezes aliyefika Ikulu kwa ajili ya kujitambulisha.
Katika maenelezo
yake Dk. Shein alisema kuwa Zanzibar na
Msumbiji zina historia kubwa kutokana na
wananchi wa nchi mbili hizo kuwa na uhusiano na mashirikiano ya muda mrefu.
Dk. Shein alisema
kuwa sekta ya biashara kati ya Msumbiji na Tanzania imeweza kuimarika kutokana
na wananchi wa nchi mbili hizo kupata fursa nzuri ya kufanya biashara na
kusisitiza haja ya kuimarisha zaidi sekta hiyo pamoja na sekta nyenginezo.
Aidha, Dk. Shein
alimueleza Balozi huyo haja ya kuwepo kwa mashirikiano kati ya Msumbiji na
Zanzibar katika kuimarisha zao la mpunga kupitia kituo cha Utafiti kiliopo
Kizimbani Zanzibar.
Alisema kuwa
kutokana na nchi hiyo kupata mafanikio makubwa katika kilimo hicho itakuwa ni
jambo la busara kuwepo kwa mashirikiano ya pamoja.
Sambamba na hayo,
Dk. Shein alisema kuwa mafanikio yaliopatikana kwenye sekta ya uvuvi nchini
Msumbiji ni ya kupongezwa na kueleza haja ya kuwepo mashirikiano na Zanzibar
katika kuimarisha sekta ya uvuvi hapa nchini kwani tayari juhudi mbali mbali
zimeweza kuchukuliwa na Serikali ya Mmapiduzi Zanzibar katika kuimarisha sekta
hiyo.
Nae Balozi Menezes alipongeza uhusiano na ushirikiano
uliopo kati ya Msumbiji na Zanzibar na kuahidi kuendelezwa na nchi yake sambamba
na wananchi wa nchi hiyo ambao wamekuwa na mahusiano mazuri na ya kihistoria na
wananchi wa Zanzibar.
Balozi Meneza
alipongeza juhudi zilizochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya
uongozi wa Dk. Shein na kueleza matumaini yake ya kuendelezwa kwa uhusiano na
ushirikiano kati ya pande mbili hizo.
Pamoja na hayo,
Balozi huyo alitumia fursa hiyo kumueleza Dk. Shein mafanikio ya kisiasa
yaliofikiwa nchini Msumbiji sambamba na mafanikio ya uchaguzi mkuu uliofanyika
hivi karibuni nchini humo.
Rajab
Mkasaba, Ikulu
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment