Habari za Punde

Ofisi ya ZFA Taifa Ikiwa na kofuli

Ofisi ya Chama cha Mpira Zanzibar ZFA ikiwa na kofuli baada ya kuamriwa na Mahakama viongozi wake kusimamishwa na kuamriwa kuchanguliwa Uongozi wa muda, baada ya mmoja wa Kiongozi Makamu wa Rais ZFA Zanzibar Alhaj Haji Ameir Haji, kufungua kesi mahakamani.

Viongozi waliozuiliwa ni Rais wa ZFA Taifa Ndg Ravia Idarous,Makamu wa Rais ZFA Pemba Ndg, Ali Mohammed na Katibu Mkuu wa  ZFA Ndg.Kassim Haji.
Pia Mahakama imeagiza kuzuiya kwa muda akaunti mbili za ZFA, zilioko PBZ na KBC.
Pia wamezuiliwa kujiingiza kuingia katika masuala yoyote yanayohusu ZFA, hadi hapo zuio lililofunguliwa na walalamikaji litakaposikilizwa pande mbili pamoja.na kutoshiriki katika utayarishaji na matumizi ya Katiba mpya ya Chama hicho.
Mahakama imemuagiza Mrajisi wa Vyama vya michezo kuunda Kamati ya Muda.itakayosimamia masuala ya ZFA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.