Habari za Punde

Balozi Seif Awahutubia Wananchi wa Nungwi na kutoa Vifaa kwa Vijana na Vikundi vya Wanawake Nungwi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozio Seif Ali Iddi akikabidhi seti za Jezi kwa Timu 9 zilizomo ndani ya Jimbo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja akitekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2010  iliyoahidi kuimarisha sekta ya michezo nchini.
 Balozi Seif akikabidhi Seti za TV na Mashine za DVD’S kwa Maskani 11 zilizomo ndani ya Jimbo la Nungwi ili kuwapa fursa wana CCM na Wananchi wa Jimbo hilo kupata Habari, Matukio pamoja na Burdani zinazotokea Nchini na zile za Kimataifa.
Balozi Seif akikabidhi Seti za TV na Mashine za DVD’S kwa Maskani 11 zilizomo ndani ya Jimbo la Nungwi ili kuwapa fursa wana CCM na Wananchi wa Jimbo hilo kupata Habari, Matukio pamoja na Burdani zinazotokea Nchini na zile za Kimataifa.
Wana CCM wa Jimbo la Nungwi wakionyesha sura za furaha baada ya kupokea msaada wa Seti za TV na Mashine za DVD’S zilizotolewa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Wanan CCM wa Jimbo la Nungwi baada ya Kuweka Jiwe la Msingi la DR. Omar Ali Juma Maskani hapo Nungwi.
Baadhi ya WEana CCM wa Jimbo la Nungwi wakifuatilia hotuba ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif hayupo pichani alipozungumza nayo katika mkutano wa hadhara baada ya kuweka jiwe la msingi la DR. Omar Ali Juma Maskani Kijijini Nungwi.
 Vijana wa Kikundi cha Kuhamasisha cha Mchikichu cha Nungwi kikifanya vitu vyake kwenye mkutano wa hadhara wa CCM Jimbo la Nungwi ulioambatana na kupatiwa Seti za TV na Jezi kwa Maskani na Timu za Soka za Jimbo hilo.
Mama Asha Suleiman Iddi akiwatahadharisha wana CCM na Wananachi wa Nungwi kuwa kuwa macho na wanasiasa matapeli walioanza udalali katika maeneo mbali mbali nchini.(Picha na Hassan Issa OMPR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.