Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Jean Sherlock, ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na ujumbe wa Ireland uliofika ofisini kwake Migombani.Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisisitiza jambo wakati akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Jean Sherlock, ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland Jean Sherlock, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani. Kulia ni Balozi wa Ireland nchini Tanzania bibi Fionnuala Gilsenan. (picha na Salmin Said, OMKR)
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amekutana na kufanya mazunguzo na ujumbe wa Ireland ukiongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wan chi hiyo bwana Jean Sherlock.
Katika mazungumzo hayo, Maalim Seif amesema Zanzibar bado inahitaji kushirikiana na washirikia wa maendeleo ikiwemo Ireland katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Amefahamisha kuwa Zanzibar ikiwa nchi ya visiwa, tayari imeshuhudia athari mbambali zitokanazo na madiliko ya tabia nchi, ikiwemo maji ya bahari kuingia katika maeneo ya kilimo na kuyafanya maeneo hayo kushindwa kutumika kwa shughuli za kilimo.
Ameyataja maeneo mengine ambayo Zanzibar ingeweza kushirikiana na Ireland kuwa ni pamoja na kilimo cha umwagiliaji, msongomano wa wanafunzi madarasani pamoja na maendeleo ya Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA).
Akizungumzia kuhusu hali ya siasa nchini, Maalim Seif amesema Zanzibar iko salama na itaendelea kutunza na kulinda amani iliyopo, ili kuwawezesha wawekezaji kuendelea kuishi na kufanya shughuli zao bila ya hofu.
Kuhusu uchaguzi mkuu ujao, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amesema ipo haja ya kuwepo waangalizi makini wa kimataifa katika mchakato wa uchaguzi, ili kushuhudia hali halisi ya siasa za Zanzibar.
Nae Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ireland bwana Jean Sherlock ambaye aliambatana na balozi wa nchi hiyo nchini Tanzania, amesema Ireland itaendelea kushirikiana na Zanzibar katika kuendeleza miradi yake ya maendeleo.
Bwana Sherlock amesema Ireland inajivunia uhusiano mwema uliopo kati yake na Zanzibar, na kwamba kuna haja ya kuimarishwa zaidi katika maeneo tofauti kwa maendeleo ya nchi zote mbili.
No comments:
Post a Comment