Habari za Punde

Kamati Maalum ya CCM Zanzibar Yapitisha Jina la Dk.Shein,Kugombea Urais kwa Tiketi ya CCM Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2015.

 Mjumbe, Dkt.Bilal, akimpongeza Dkt. Shein baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe katika Kikao cha Kamati Maalum ili kugombea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal wakiwa katika ukumbi wa mkutano baada ya kuingia Makamu Mawenyekiti wa CCM. 
 Wajumbe wa Mkutano wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar wakimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Shein, akiingia katika ukumbi wa mkutano. 
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndg Vuai Ali Vuai akizungumza wakati wa Kikao hicho Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. 
Makamu  Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt. Mohamed Ali Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar (hawapo pichani) wakati wa kikao cha Kamati Maalum ya CCM kilichofanyika leo Julai 5, 2015 kwenye Ukumbi wa Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar kwa ajili ya kujadili na kupitisha jina la Mgombea Urais wa Zanziba kwa Tiketi ya CCM. (katikati) ni Mjumbe wa Kamati hiyo, ambaye aliongoza kikao baada ya kuteuliwa kuwa Kaimu Mwenyekiti, Dkt.Mohammed Gharib Bilal na Mjumbe, Balozi Iddi.


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dkt.  Ali Mohammed Shein, akizungumza na Wajumbe wa Kikao cha Kamati Malum, akiwashukuru baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe hao kugombea Urais wa Zanzibar, katika Kikao kilichofanyika leo Julai 5, 2015 kwenye Ofisi za CCM Kisiwandui mjini Zanzibar. 

Wajumbe walioshiriki katika Kikao hicho.cha Kamati Maalum ya CCM Zanzibar kupitisha jina la Mgombea wa CCM Urais Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa mkutano.

Kaimu Mwenyekiti wa CCM, Dkt.Mohammed Gharib Bilal, akiendesha Kikao hicho maalum cha Kamati Maalum, baada ya kuteuliwa na Wajumbe wa Kamati hiyo. Kushoto) ni Balozi Seif Iddi.kutangaza jina la Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM, 



Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati Maalum ya CCM Zanzibar nje ya jengo la CCM.





No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.