Habari za Punde

Mdahalo wa siku moja wa jukwaa la amani na utulivu, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wafanyika Pemba


MWENYEKITI wa mwenvuli wa asasi ya kiraia Pemba, ‘PACSO’ Omar Ali Omar akifungua mdahalo wa siku moja wa jukwaa la amani na utulivu, wakati na baada ya uchaguzi mkuu, uliotarayarishwa na asasi hiyo, na kufanyika skuli ya Sekondari ya Fidel Castro, kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa ‘PACSO’ Ali Said Hamad na katikati ni Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC, tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
MRATIBU wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed, akiwasilisha mada ya umuhimu wa amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu, kwenye mdahalo ulioandaliwa na asasi ya ‘PACSO’ kulia ni Mkurugenzi mtendaji wa asasi hiyo, Ali Said Hamad na kushoto ni Mwenyekiti wake Omar Ali Omar, mdahalo huo umefanyika skuli ya sekondari ya Fidel Castro, (Picha na Haji Nassor, Pemba)  
WASHIRIKI wa mdahalo wa jukwaa la amani na utulivu wakati na baada ya uchaguzi mkuu, lililoandaliwa na Mwenvuli wa asasi za kiraia Pemba, PACSO, na kufanyika skuli ya sekondari ya Fidel Castro Chake chake Pemba, wakisikiliza mada inayotolewa, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
MSHIRIKI wa mdahalo Hidaya Mjaka Ali, kutoka Jumuia ya watu wenye ulemavu Pemba, akichangia mada juu ya umuhimu wa amani, katika mdahalo huo, uliofanyika skuli ya sekondari ya Fidel Castro, na kuandaliwa na asasi ya ‘PACSO’ Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba)
SAJENT Hamad kutoka Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba, akielezea jinsi jeshi hilo lililovijipanga kulinda amani na utulivu, wakati na baada ya uchaguzi mkuu, aliekuwa kwenye mdahalo wa jukwaa la amani na utulivu, uliotayarishwa na asasi ya PACSO na kufanyika Skuli ya Fidel Castro Chake chake Pemba, (Picha na Haji Nassor, Pemba). 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.